Dear Ankal,
Kwanza nikupe Big UP!!! sana kwa kuendesha blog yetu kwa weledi wa hali ya juu. Yaani ma-news kila dakika na up-to-date kama CNN mwanangu. Hakika unatisha na hakuna wa kukufikia kaka. Halafu unanikoshaga kwa kutoweka mambo ya udaku, umbea na majungu...

La pili ni kukupongeza kutoa nafasi kwa wadau kutoa madukuduku yao bila chenga. Yaani yule jamaa wa juzi wa Norway anayepima zali la kuja kuomba visa ya Marekani baada ya kuopoa Green Card ni funika bovu. Ndio maana na mimi leo najikunja kuomba ushauri toka kwa wadau wako lukuki duniani kote, japo shida yangu ni tofuti na ya mdau wa visa wa Norway ambaye nami namshauri asinoe stepu na kuhamia Marekani. Mie niko huku mwaka wa 28 leo, na Green Card yangu, lakini acha! Kufa sifi ila cha moto nakiona. Nna kila kitu ila sina mwenza wa kufurahi nae...

Mie Ankal naishi East Coast huku (kwa sasa jina la mji kapuni, wambea naogopa wasinichore). Tatizo langu natafuta mwenza kutoka nyumbani Tanzania, tatizo sijafika huko miaka yote hiyo na pa kuanzia sijui (wazazi wangu wote wametangulia mbele ya haki). Ndugu zangu wengi nimepoteza mawasiliano nao (waliniliza pesa nilizowatumiaga za kujengea, wamezila na wakakata mawasiliano) hivyo sina uhakika kama wote wapo. Nilikuwa naishi Kariakoo, Dar, mtaa wa Narung'ombe, ila katika taswira moja ulioonesha siku za hivi karibuni nimeona nyumbani petu pana bonge la kikwangua anga. Najua tu kuwa jamaa zangu ndio wameshauza nyumba yetu na kulala mbele.

Samahani kama nawakwaza kwa hadisi ndefu ila shida yangu ndiyo hiyo. Nataka kurejea nyumbani mara moja kuja kusaka wa kuishi naye. Mie sasa nagota miaka 51 ila bado niko fiti kila idara, ikiwa ni pamoja na pesa ya kubadili mboga kila siku hainipigi chenga. Maana boxi ninalokula huku si haba. Niliwahi kuishi na mfilipino na baadaye Mvenezuela lakini tukazinguana sasa niko alone. Mfilipino nilizaa naye watoto wa kiume wawili, kakimbia nao kwenda wapi sijui. Huyu mwingine hatukubahatika.

Sasa basi, shida yangu ni wapi pa kuanzia pindi nikija huko???  Halafu huyo mchumba, ambaye sina tatizo la dini wala elimu yake (awe na angalau ya fom foo tu, tosha!), nitampataje wakati nikija nitakuwa mgeni na muda wangu ni wiki tatu tu???

 Naomba mchango wa mawazo toka kwa wadau nifanyeje nipate mwenza wa Kitanzania toka nyumbani Tanzania?? Nikija nianzie wapi?? Kuna agency za kutatua matatizo kama hayo huko???

Mdau
East Coast, USA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2013

    Bongo mademu wengi ila walio makini na wanahitaji ndoa wanajali sana suala la dini sijui wewe dini gani ni vema useme. Huku wasichana wengi sana kuliko wanaume but kweli uwe serious Michuzi atakusaidia.
    Mabinti wa kichaga, kihehe, kibena,waluguru, wafipa, wapare wa mwanga huko ugweno na usangi, wamasai hadi sasa bado wanashika chati kwa kumudu familia zao vema. inategemea pia na malezi fuatilia suala la dini na ndoa za wazazi wao pia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2013

    MIMI NI MSICHANA WA KITANZANIA,UMRI NI MIAKA 34 NI MWALIMU WASHULE YA MSINGI.MIMI NI BIKIRA NAPIA NIMEOKOKA.WEWE UMESHAISHI NA WANAWAKE WENGINE HUKO JE?NITAKUAMINI VIPI MTU KAMA WEWE?NIPE MAWAZO.MIMI NIPO MARANGU MOSHI ,MCHAGGA WA MWIKA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2013

    Haaa michuzi atamsaidia??? yaani kazi yake kuunganishia wapenzi au? Mwombe Mungu wewe mzee wa 50's! pesa ya kubadili mboga wala kuwa USA haijalishi! unaweza kupata Mtanzania naye akakukimbia tu! kwa nini hao walikukimbia???

    ReplyDelete
  4. ChakubangaMay 10, 2013

    Kwa ushauri wangu kama unajamaa unao waamini waambie wakutafutie kama wanawake 3 ambao wanawafahu vya kutosha ya kuwa na sifa za kuwa "future wife" bila ya wao wahusika kufahamu, ukifika omba kuonana nao just kwa maongezi bila ya kuwa moja kwa moja unaonyesha nia ya kutafuta mchumba, if possible hata wasijue umetoka America, waweza zuga kwamba umekuwa ukiishi Kenya/Uganda, then out of those three you can make decision who to take to the next step, from there then ndio ukampa full story wewe ni nani na umetoka wapi.

    Sababu ya kusema hivyo ukiingia kichwa kichwa Bongo wadada wakijua umetoka Mtoni waweza kujikuta umeoa changudoa aliye ficha makucha na soon akifaika America jiandae kukimbiwa na kuacha mpweke tena na possible na virusi vya ukimwi.

    Kama huna any reliable people in Tanzania, kwa ushauri wangu forget it na jitafutie mwenza huko huko, Please my friend you have been abroad for a long time for should have experience, si lazima kupata some one from Tanzania,kama ni mwafrika waweza pata huko huko, there are nice and respectiful women from Gambia,Sierra Leone, Kenya,Ghana etc go for them, who told you the best wife must come from Tanzania !

    Huo ndio ushauri wangu. If you want more advise let me know your e-mail then I can give more mature people piece of advise, I am almost your age and lives abroad and was in almost similar situation like yours

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2013

    Duh!!! umeoa mpaka wafilipino?
    Wenzako wapilipino wanawafanya watumishi wa kazi za ndani, wewe umekwenda kuoa kaka?

    Nakushauri tafuta Akata mmoja, (mnugu), ishi naye. Wanawake wa bongo wewe huwawezi tena.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2013

    WEWE FALA WA HUKO SIJUI EAST COAST HAYO MAMBO YA MAJIVUNO HAPA HAPA BONGO NI KAMA USA NA DOLLARS NI PESA INAYOTUMIKA KILA SIKU BONGO! WALA HAUNA FALA MWANAMKE AACHE SHUGHULI ZAKE HUKU ATI AJE AOLEWE MAREKANI KWA MTU KAMA WEWE MPIGA BOX , SIKU UKIKOSA DAY WORKER BASI NJAA IMEINGIA NDANI NO NO NO HUPATI MTU,

    MIAKA 28 HUJAFIKA BONGO NJOO KWANZA UANGALIE MAENDELEO YA BOMGO NA UONE WATU WANAVYOISHI NDIO UTANGAZE MATANGAZO HAYO YA KUTAKA MCHUMBA. HAKUNA USHAMBA HUO TENA WA MAREKANI SIKU HIZI HATA RAIS WAKO WA ZAMANI KABLA YA OBAMA ,GEORGE BUSH ANATAKA HAMIA HUKU TAYARI ANA MBUGA NA NYUMBA ANAJENGA, HIO NALUNGOMBE UNAYOIONA KWENYE PICHA NI SOKNI TU HAPO BADO MJI HUJAUONA .

    JARIBU WAULIZE WABONGO WENZAKO HUKO KAMA WANA DADA WAKUUNGANISHIE HUKO HUKO ITAKUWA RAHISI KWAKO NA MAISHA YAKO NA MKEWE MPYA

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2013

    Mbona mtoa maoni mnamba moja umewasahau dada zetu wa kihaya? Ubaguzi siyo mzuri mdau.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2013

    Nenda Pemba ukisema tu kama wewe umetokea USA na makaratasi unayo utapewa mtoto wa Kiarabu bikra lakini ukubali kusilimu kama si Muislam!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 10, 2013

    shughuli anayo miaka 51 cmchezo maana hapo kwa hesabu ya haraka ni kwamba ampate si binti mdogo bali mkubwa mwenzie wa kuliwazana,maana kwa suala watoto si mtoto atamwita babu muda mfupi tu aangalie vzuri suala hili asije kosea labda kama anatafuta wa kurithi mali zake

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2013

    Nenda kasimame pale posta ya zamani

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 10, 2013

    Kaka yule mdau wa Norway anayetaka kwenda Marekani,hajui analofanya-maana Norway ni safi sana kushinda hata hapa Marekani-sisi wenyewe tulio hapa Marekani tunatamani kwenda NoRWAY KUISHI.

    Kaka ukipata msichana wa nyumbani oa,sema nenda nyumbani utawaona.Hakuna mzuri,omba upate neema ya mwenyezi Mungu uweze ishi naye.
    Wewe ukipata likizo nenda bongo-achana na hawa wa mtandaoni,wengi ni wanafiki tu.
    Hongera sana kaka kwa kuwa mwazi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 10, 2013

    Mwenzenu ana shida. Kwa nini mnamchora hivyo. Wote aliowaoa hawakuwa waafrica. Nyie mnajua jinsi waafrica wanavyodharauliwa out of Africa? Tafuta mke kaka Mungu atakuzawadia. Ila sasa, mambo ya kutojieleza vizuri nayo siyo mazuri. Namfahamu mama fulani ambaye naye anatafuta mtu wa kuishi naye, ila lazima awe mcha Mungu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 10, 2013

    50yrs na bado hujaoa????? kweli maisha ya sasa ni ya ki-digital, haya me nimeachika na mtoto 1 utanikubali?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2013

    Huyu hana Baraka! Mtu asiyejali Dini ya Mchumba? Wapo wanaoamini Miungu. Hao nao unawataka.

    Tangu lini Uchumba ukapatikana kwa wiki 3! Unatafuta Malaya au Mchumba?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 10, 2013

    Huyu "mchumba" angeweka email yake wanawake tujitose kama vile tunaomba kazi then atachuja na hapo atajua pa kuanzia na hatimae ampate mwenza wake. Tunaomba email yake watu tufanye application tafadhali.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2013

    mi nafikiri kwa kuwa unampango wa kuja,njoo uchague mwenyewe maana ni wengi mno inategemea tu na mtu unayemtaka,kama unataka sura nzuri,nitakupa maeneo ya kufanyia hiyo risechi yako,simama maeneo ya posta kuanzia mida ya saa kumi jioni,kituo cha daladala cha akiba (EBE),kituo cha daladala cha ardhi,au kasimame feri saa za asubuhi na jioni.Kwa maeneo haya machache bro. utakimbia mwenyewe.

    ReplyDelete
  17. Mbona easy sana tu? wala usipate shida wewe ukifinga Bongo nenda pale Jolly Club Upanga ni bwerere mke umepata ni wewe ndugu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2013

    Angalia usije ukapata anger and disappointment kwa huyu Mtanzania utakayepata/patiwa kwani watakufirisi hizo US.Dolla zako kwani umesha tangaza kuwa michuzi unayo.Tanzania ya zama zile siyo ya sasa,mengi yamebadilika,siku hizi wasichana wenyewe ndio wanatongoza wanaume(niulize mimi..miguu begani nilikuwa nawakimbia)pia sasa dini yako
    na umri,ndugu watakuja wenyewe tena kukufirisi au kukuroga ili wachukue mali zako tena,njoo na bunduki yako, majambazi mengi zaidi ya police.Kwa nini usioe na kuchukua mke to USA,huko wewe sasa ni kama samaki kwenye maji.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2013

    Nakupongeza sana kwa kuwa muwazi na kutafuta ushauri. Ila kaka, hivi kweli unavyosema unatoka US na unavijipesa unatagemea nini? Kama una nia kweli ya kupata mke mwema jamani onesha upo serious...weka personality yako hapa, pesa zinakuja na kuondoka! Wanawake unaodhani utawa impress kwa sehemu unayoishi na pesa ulizonazo siyo wanawake wanaostahili kuwa "mke". Nina uhakika kuna wamama wengi tu ambao wangeweza kuwa "mke mwema" kwako ila kwa jinsi ulivyojieleza hawawezi hata kuthubutu kukutafuta. Tafadhali unesha nia! Kila la kheri.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 10, 2013

    Wewe Mchaga mwenye bikira Mlokole wa Mwika Mtoa Maoni wa No.2 hapo juu:

    .....................
    MIMI NI MSICHANA WA KITANZANIA,UMRI NI MIAKA 34 NI MWALIMU WASHULE YA MSINGI.MIMI NI BIKIRA NAPIA NIMEOKOKA.WEWE UMESHAISHI NA WANAWAKE WENGINE HUKO JE?NITAKUAMINI VIPI MTU KAMA WEWE?NIPE MAWAZO.MIMI NIPO MARANGU MOSHI ,MCHAGGA WA MWIKA.
    ....................

    Hivi wewe ktk kasi ya Maisha yetu haya umri wa miaka 34 bado tu unayo bikira?

    Acha uongo, Mdau atakuitia Mabibi Wazee wakukague sio kwa sababu unasikia jamaa yupo Marekani wewe Mlokole wa Mujini unakwenda Sokoni Kariakoo au Sokoni kiboriloni Moshi kununua Bikira bandia ili upate nafasi!

    Wakati wewe ni mwalimu na ulishapitia Vyuo vya Mabweni na maisha mchanganyiko.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau wa East Coast Marekani.

    Kutafuta mwanamke Bongo uwe makini sana ama sivyo utapata Mcheza Taarabu mwanamke wa mipasho atakaye kupa presha ya maisha na maisha mabovu na vile wanasikia wewe upo Marekani.

    Unaweza kumchukua mwanamke akiwa Kondoo lakiniafiki ile anakanyaga Marekani kutoka Bongo anakuwa Chui anakugeuka anakuwa Changu, anakuwa Mcharuko anakuwa Jamvi la wageni usije shangaa anatoa hadi kwa rafiki zako!

    Bongo wanawake ni wengi kama Mdau wa kwanza anavyosema isipokuwa wengi hawaoleki na hawana sifa za kuitwa Mke!

    Hujaambiwa ?,,,kwa sasa Wanawake wengi wa ki-Bongo wanapenda pesa na maisha ya juu lakini hawapo kwa penzi la ukweli.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau wa East Coast jihadhari sana utakalia kuti kavu Bongo!

    Ni afadhali TANGAZO LAKO HILI UNGELITOA UKIWA UMESHAFIKA BONGO TENA UKALITOLEA KANISANI AMA MSIKITINI!

    Pana hatari usipate mtu anayestahili, ukapata mwanamke Galacha, Mcharuko, Guberi ama Gwinji. !!!

    Bora uolee huko huko Marekani, pana jamaa alikuja chukua mwanamke Bongo alijuta kuzaliwa!

    Mwanamke kufika Marekani alimgeuka, hakuamini akaolewa na Mzungu!

    Wapo Wanawake wazuri kwa tabia na sura wamejaa Bongo lakini kuwapata ni bahati sana, inategemea na Mawakala wako akina Dada watakao kuunganisha.

    Wengi wa madada wa Kibongo ni
    :-

    -Wavivu.
    -Tegemezi, wanapenda maisha ya juu.
    -Malaya ni wengi sana, wana tabia mbaya ya kuwa na wanaume wengi wakiona kuwa kupendwa na wengi ndio uzuri wenyewe.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau Mnyamwezi wa East Coast!

    Ohooo Wanawake wa Kibongo uawaweza wewe?

    Mwanamke mmoja ana wanaume 10 au zaidi,,,simu yake anasevu majina ya wanaume kwa kuweka ya kike.

    Wengi hawaoleki, ila wakisikia Tangazo lako watafika makucha wakijifanya Kondoo wakati wao ni Chui.

    Wanawake wa Kibongo watakufanya ufe haraka ama kuzeeka haraka kwa mawazo na mfadhaiko wa kiroho!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 10, 2013

    Mnyamwezi wa East Coast!

    Wanawake wa Kibongo wanapenda ngono zembe na wanapenda uzazi bila mpango!

    Je, utaweza?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 10, 2013

    ushauri wangu kaka fika kwanza tanzania then date na msichana but usijiexpress kwamba unataka kuoa au unaishi marekani then uchunguze tabia yake baada ya hapo ndio utajua miolewaji ni nani na nani mtumiaji, pia jiweke kwamba hauko mambo safi manake kuna watu wako interested na pesa tu.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau,chukua huyu hapa:Fungua Biblia,kitabu cha Mithali sura ya 19:mstari wa 14,inasema:"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara,mtu hupewa na BWANA".Hao wengine ulijitafutia mwenyewe kwa akili zako,matokeo yake hawakudumu.Sasa badili mbinu za utafutaji,nenda kwa staili niliyokupa hapo juu,utapata mke mwema.Mungu akupe ufahamu uuone ukweli huo.Kumbuka kwa Mungu yote yanawezekana.Kila la heri.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau,chukua huyu hapa:Fungua Biblia,kitabu cha Mithali sura ya 19:mstari wa 14,inasema:"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara,mtu hupewa na BWANA".Hao wengine ulijitafutia mwenyewe kwa akili zako,matokeo yake hawakudumu.Sasa badili mbinu za utafutaji,nenda kwa staili niliyokupa hapo juu,utapata mke mwema.Mungu akupe ufahamu uuone ukweli huo.Kumbuka kwa Mungu yote yanawezekana.Kila la heri.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 10, 2013

    Vp kaka,
    Naomba e-mail yako nitakuunganisha na mdogo wangu anaishi huko huko Marekani - ila hana makaratasi. Ana tabia nzuri sana and will be right age for you.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 10, 2013

    Mnywezi wa East Coast.

    Tanzania hakuna mwanamke mbaya siku hizi hasa Jijini Darislama, kila umonaye ni mzuri MCHINA ameshika kasi sana, kuna hadi MAKALIO, KUCHA, KOPE, MAPAJA NA RANGI ZA NGOZI kazi kwako unaweza pata mzigo wa kuchakachua usiokuwa Orijino.

    Hio haitoshi wanawake wanapaka LIPSTICK hadi kwenye kope za macho, sehemu kama Kariakoo kwenu pale!

    Pana Bikira za kufoji zipo ktk masaluni ya kike.

    Kama unataka mwanamke wa ukweli labda ushitukize kumuibukia alfajiri akiwa anatoka Kitandani na kabla hajakaa ktk Kioo na kujirembua!

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 10, 2013

    Miaka 51 tu?

    Nani alikwambia mtu akiwa na mika 51 ndio hana uwezo wa kiume?

    Kwa taarifa yako pana wazee wana zaidi ya miaka ZAIDI ya 78 lakini bado wapo fit,

    MWANAUME ANAZEEKA AKIINGIA KABURINI TU!

    Ulisikia wapi wanaume wakizeeka hadi uwezo wa kimwili?

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 10, 2013

    Ndugu yangu siku zote mambo mazuri hayakosi misukosuko,kwa hiyo usishangae hao wanoa taka kukukatisha tamaa, kama ni wanaume/ wanawake wajiulize wao wameoa/wameolewa wapi? kama hakuna wakuoa hapa? Kila jambo jema hupangwa na mungu. kwa hiyo wala usikate tamaa, We njoo uchague mwenyewe na kama huna ndugu sidhani watz wamekuwa na roho za ajabu mpaka washindwe kukusaidia, ninavyojua watanzania ni wema na wakarimu sana.Na isitoshe kwa mtu kama wewe ambayo umeshajiweka wazi

    Jaribu kuwa mbali na wanao kukatisha tamaa. siku zote wabaya hawapendi jambo zuri la mtu lionekane linapendeza.

    Mungu akutangulie

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 10, 2013

    Kaka kazi kwako kunakigoli hapo changamka uje umfate miaka 51 na 34 sio mbali sana fanya fasta kabda hawajakuwahi kutoa kabikira kake.
    una raha weye unapata msichana bado hajaguswa. te te te te te ter

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 10, 2013

    Unashangaa mtu wa miaka 51 hajaoa?

    NDOA ni rahisi?

    ;;;;;;;;;

    50yrs na bado hujaoa????? kweli maisha ya sasa ni ya ki-digital, haya me nimeachika na mtoto 1 utanikubali?

    ;;;;;;;;;

    Wewe mtoa Maoni akili yako siyo nzuri!

    Wewe unafikiri woooote wasio ktk ndoa ni kwa uzembe wao?

    Ndoa ni kitu kigumu sana, na wala usije kuona mtu akiwa na mri mkubwa akiwa hana ndoa, na ndio maana kwa wenye busara panapokuwa na mgogoro wa maelewano ktk ndoa, Wasimamizi wa suala hawakimbilii kuivinja ndoa bali wanajadili jinsi ya kuijenga na kuiimarisha ka kutumia busara zaidi.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 10, 2013

    Mnashangaa mtu wa miaka 51 mkisema kazeeka?

    Ehhh!

    Pana jamaa mmoja alipata safari ya Masomoni nje kwa miezi 6 tu, akamwaggiza Babu yake umri miaka zaidi ya 80+ Kijijini akamwacha kwake Mjini asimamie familia yake.

    Jamaa alipomaliza Kozi kurudi TZ alimkuta mkewe wakiwa Mjamzito!

    Alipomuuliza mkewe na kumbana mke akamwambia muulize babu yako.

    Jamaa kumbana babu akakubali!

    Sasa jamaa ilibidi pumzi zimshuke chini, kwa kuwa mimba imejazwa na babu yake mzaa baba ambaye jina lake la mwisho ndilo anatumia jamaa!!!

    Hakuwa na jinsi ilibidi alichukulie tukio lile kuwa babu ameongeza ukoo!!!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau wa Marekani:

    Mwanamke wa Kibongo ni Kunguru hafugiki!

    Wengi wa Wanawake wa Kibongo wana sifa hizi chafu chini.

    1.Washirikina NA hawajiamini,
    WENGI WANAISHI KTK IMANI ZILE, UNAWEZA KUKUTA MWANAMKE TENA MSOMI NA MWENYE KAZI NZURI LAKINI KILA WIKI ENDI ANAHANGAIKA KWENYE VIBANDA VYA AKINA BABU USAKA NDUMBA.

    2.Tegemezi,
    WANAWAKE WENGI WA KIBONGO HATA KAMA AKIWA NA KAZI YENYE KIPATO KULIKO MUME LAKINI BADO ATAMTEGEMA MUME, NA IKITOKEA MUME HAWEZI BASI MKE ATAMMNYANYASA SANA MUME KWA UWEZO WAKE KUWA CHINI KIFEDHA NA MARA NYINGI NDOA HULEGA LEGA AMA HUVUNJIKA KABISA KUANZIA HAPA.

    3.Wavivu,
    WENGI WA WANAWAKE WA KITANZANIA NI WAVIVU HATA KWA KUFIKIRI. HUPENDA KUFIKIA MALENGO KWA NJIA ZA MKATO. HAWAPO TAYARI KWA CHANGAMOTO ZA MAISHA YA DUNIA YETU YASIYOTABIRIKA.

    4.Akili ndogo kuhusu hatma ya baadae,
    WENGI WA WANAWAKE WA KIBONGO HAWANA UPEO WA KUCHANGANUA MAMBO HASA INAPOFIKIA KUHUSU HATMA YA BAADAE KIMAISHA.

    5.Hawaaminiki,
    ANAWEZA KUTEMBEA NA YEYOTE ILI MRADI MASLAHI, AU MARA ZINGINE HATA KAMA HAPATI KITU ILI MRADI TU AGAWE NA KUKUKOMOA WEWE MUME!

    Angalia sana ndugu HATUKUTISHI ISIPOKUWA TUNAKUFUNGUA MACHO BAADA YA SISI KUTUFIKA MAKUBWA MAISHANI MWETU ktk mchakato wako kutafuta mke usije ukanasa pabovu!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 10, 2013

    Mwanamke wa Kibongo atakuletea stress na Kisukari!

    Wewe kukaa kwako Majuu muda mrefu wanawake wa Kibongo huwawezi yatakufika kwa kuwa wengi sio wakweli.

    Utajikuta unapata presha na kisukari au ukafa mapema!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 10, 2013

    Una miaka 51 tu?

    Kwa kuwa ktk ndoa na Mwanamke wa Kitanzania utazeeka kwa kasi ya ajabu hadi mwaka mmoja (1) ndani ya ndoa utaonekana kama una umri wa Kaka yake Marehemu Bi. Kidude miaka (Mia moja na Kumi na Tano) 115 !!!

    Chezea wanawake wa Kibongo wewe?

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 10, 2013

    ndugu yetu wa Marekani,

    achana na wanawake mzigo, majanga na walio shindikana wa Kitanzania tafuta mwanamke hukohuko Majuu huku njoo na Mipango ya Uwekezaji ktk Gesi, mafuta na Madini.

    Katibu sana Tanzania!

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 10, 2013

    Hongera mdau kwa kufikia hatua hiyo ya kuhitaji mwenza, pia pole kwa yaliyokukuta. ni kweli maisha ya ss yamebadilika sana.Ni kazi ngumu sana kama ukiwa hauko serious lkn ni kazi rahisa sana ukiwa serious. ya kupasa uwe makini sana. sijajua dini yako, ila mshirikishe sana mungu ktk suala hili.nimependa ulivyoamua kuweka wazi maisha yako japo si sanaaaa. Umri si tatizo kwa mtu ambaye amedhamiria kuishi maisha ya ndoa na mwenye mapenzi ya dhati. tatizo ni 'UPENDO", NA "UVUMILIVU". Sijajua unahitaji mweza mwenye umri gani. mm ni mmojawapo wanaohitaji mwenza wa maisha.karibu sana ukija tena TANZANIA.

    ReplyDelete
  40. We mdau mtafuta mke.........Wewe ni mzembe, yaani unakaa na mwanamke mpaka mnazaa watoto wa2, halafu anakimbia nao halafu kwako ni poa tu...dah. Sasa ndo umekumbuka shuka kukiwa kunakucha, kwenye age ya 50s utaweza kulea mke? Halafu watoto....dah, potelea mbali achana na hiyo kazi, baki tu mseja, in fact umri wenyewe umebaki 20years wa kuishi.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 10, 2013

    Mimi ni dada yako wa miaka 54 sasa.
    Ninakuomba uniandikie email ili nikuunganishe na wa dada wenye hofu ya Mungu na nina sali nao utaongea nao wewe mwenyewe na kisha utaamua uchague nani kati ya watu mbali mbali waliokuandikia
    ak_abduel@yahoo.com

    ReplyDelete
  42. NI HATUA NZURI ULIYOFIKIA YA KUHITAJI MWENZA. KAMA HUTOJALI NAOMBA KUPATA A/C NAME YAKO YA FB AU E-MAIL ADDRESS YAKO.MM PIA NAHITAJI MWENZA.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 10, 2013

    Mdau hapa TZ sio kwa mke tu bali kila kitu. Mtu akijua tu uko majuu basi vituko, bei zitapandishwa, chako kitaibiwa, askari watatafuta kila kosa wakubambikie, ndugu nao watakupa ushauri ili wakuibie. Mnjoo hapa UK kuna wanawake wengi wazuri wa Ki-English (Weupe) hawapendi kudhulumu mwanamume pesa yake. Tena ukiwa utaishi naye USA watakupenda sana maana wamechoka na tabia za Waingereza wenzao. Anachotaka ni penzi tu. Hata mastar wa USA wanakuja hapa UK kuchukua wake.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 10, 2013

    kumpata mwenza wa kitanzania nenda tanzania wapo wengi chagua unayemtaka bana wewe mbona unakosa cha kuongea? ukiwa tanzania ndipo walipo chagua wa aina unayotaka mwenyewe unataka mawazo ya watu mengi hapa itakuwa sumu kwako.mie najua haupo siliazi.unataka uchaguliwa mke unafikiri mke/mume wa taipu yangu ndio atakuwa wa taipu yako mkuu.nenda mwenyewe tumia akili yako mwenyewe mkuu.pole sana kama unatafuta mawazo hapa.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 10, 2013

    Norway kuna Contryman anataka sana kuja US, na Norway inaruhusiwa ndoa 'of the same sex'. Hebu wasilianeni na msaidiane.

    ReplyDelete
  46. Johari,TangaMay 10, 2013

    ndugu mdau,kabla ya yote pole.
    mi nakushauri kwanza Muombe mungu kwa imani yako ,pili uwe makini sana hata ukija bongo,wanawake wengi ni sanaa tupu siku hizi,usije ukakurupuka,pia hata ukija inapidi usioe within that two weeks,labda ukifanikiwa kumpata upate tu mawasiliano nae ile umfatilie taratibu tabia.Ingawa mi pia ni mdada ila wadada wanasumbua.na ukumbuke kupima kwanza kabla ya yote.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 10, 2013

    Wewe Mu-East Coast huku Bongo hakuna anayebabaikia tena watu kutoka USA wala nchi yoyote ile. Alafu inaonekana umeshavufilia mbaya miaka 28 nje ya nchi ukija hapa utakimbia mwenyewe kwani watu wamebadilika na maendeleo ni almost the same with USA.
    Pesa Bongo nje nje watu wanafanya issues zao kwa USD tuu huku hadi Madada Poa wanataka DOLA, hivyo usibabishe watu na VIJICENT vyako tena vya kupiga BOX, yaelekea wewe bado uko nursing home unakamua PIPI TOFFEE ZA WATHUNGU. Miaka 51 uje utafute mke leo wewe ni failure kabisa na una kasoro kwani huko kuna WANUBU kibao wanalilia wanaume wa KIAFRICA wewe unashindwaje kuwapata?
    Anyway acha majivuno wewe BWEGE na wasichana huku hawakubali kabisa MAFALA kutoka USA wakijidanganyia na VIJIDOLA vyao vya pipi toffee, we umtawaze MZUNGU ndo utishe watu Ebbo! watu Bongo wana PESA BHANA za kumwaga hadi Mabinti. Kama unakuja oa is well and good njoo utafute mke na Inshaalah Mola atakujalia utapata ila usitishe watu na VIJIDOLA VYAKO UCHWARA.
    Miaka 51 uje tafuta mke leo! kweli brother??

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 10, 2013

    Mdauwa Marekani.

    Hongera kwa kuwa muwazi na pia pole kwa changamoto hii.

    Ndugu yetu wanawake wa kuolewa walikuwepo miaka hiyo ya 1985's ulipoondoka wewe hapa.

    Hasa itakapo fahamika unzo DOLLA $$$ ZA MAREKANI ohhh utabebwa mgongoni utaimbiwa nyimbo za Taarabu kitandani lakini DOLA $$$$ ZA MAREKANI zikiisha utabwagwa chini kutoka mgongoni utakimbiwa!!!

    Hivi sasa hatuna WAOLEWAJI WA KIKE tunao MAJAMBAZI WA KIKE !!!

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 10, 2013

    The best advise mshirikishe Mungu, sali, ingia kwenye Toba, funga, mwambie Mungu hitaji lako na utaona muujiza wako! Mtoaji wa Mume au Mke bora ni Mungu pekee na si mwanadamu, na Mungu anatuasi kwenye Biblia... "ALAANIWE AMTEGEMEAE MWANADAMU" anagalia ndugu yangu, kwa kutafuta mke kwa staili hii, unaweza kujikuta unaoa JINI,, shauri yako, maana shetani naye anasikia na hatakaa mbali..

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 10, 2013

    Mbona mnadhalilisha wanawake tena Huku kwa jambo na tatizo la kiume?

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 10, 2013

    Mimi naona watu wanapiga tu kelele nyingi kwa kaka watu na miaka yake 51.Kwani mbona nyinyi wabongo mnaojiita wazawa na kutukana mapato ya wezunu walio nje eti vijidola,wewe unavyo - tena usikute wewe ni house boy au kinyozi unashinda internetcafe mchana kutwa,au roho ya korosho imewajaa tu watu wazima mmekosa shughuli za kufanya kazi kulinganisha maisha yenu na ya wezenu walio nje,wakati ukweli unajuliakana nani yuko bora kimaisha kati ya mtu alifulia bongo na yule aliye nje.Mbona mnatoa kauli za kashfa,tena mkome na mkomae hii blog yetu sote , kama huna cha kusema ni bora unyamaze na uache watu wenye akili zao wachangie mawazo ya msingi, kwani eti Mengi wa IPP alivyomuoa K-lyin mbona hamkupiga kelele.Jameni muacheni kaka wa watu , kama una dada au ndugu yoyote anayetafute mume uwasiliane nae na sio kuropoka ropoka bila mpangilio.

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 10, 2013

    WEWE MDAU WA MAY 10,2013 UNAWEZA KUWA NI MROMBO,MAANA WATU WA KUTOKA HUKO WAWE WASOMI AU LAA HAKUNA KITU.ACHA KULAUMU WATU HAPA TUNASAIDIANA MAWAZO TUU.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 10, 2013

    Achana na huyu mdau anayekuita"Wewe Mu-East Coast" ni msichana inaelekea,hajui asemalo kwani anatu Dollas twa baba yake,wala hajui jinsi zinavyopatikana. Analinganisha maendeleo ya USA na Bongo!!wala hajui factors zinazo define maendeleo ya inchi(kwa vile shule hajaenda) achana naye! fuata intuation ya moyo wako inavyokuambia,ila tu usije ukaweka mayai yote kwenye kikapu kimoja!
    Au cha maana tumia pesa zako hizo kutafuta watoto wako wawili uwasaidie popote walipo(hapo US si vigumu kutafuta mtu)

    ReplyDelete
  54. Jsckson wa kahama natafuta mwanamke anae ishi na vvu umri 25-30 dini romani rc awe anaishi kahama au geita tuwasiliane-0652952240

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...