Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto) akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
 (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    jamani...pole mamii

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    Innalillah wainna ilayhi rajiuun! Jamani huyo si ni kizuka tena, mbona yu waziiii?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2013

    HIVI HAO WABABA PEMBENI WANA AKILI KWELI? KWANINI HAWAWASAIDI WAMAMA KUMSHIKA KHADIJA HUONI WAMAMA WANATESEKA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2013

    "Kullu nafsi dhaaikatul mawt" kila nafsi itaonja mauti. INNALILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2013

    Wanamama wanamsaidia mwenzao,halafu lijamaa lenye kaunda suti linakenua, wajameni, ustaarabu upo wapi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2013

    Sipendi watu wanaocheka cheka ovyo misibani!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2013

    Mdau wa 5 huyo anayekenua ukiona hivyo atakuwa ni Mtani wake Bibie Mfiwa Khadija Kopa.

    Sio rahisi mtu wa kawaida mwenye akili kukenua ktk tukio kama hilo.

    Si unaona Khadija ni wa Pwani inawekena kwa kuwepo huko Rukwa jamaa Mtani anayecheka ni wa Bara analeta Utani Msibani!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2013

    Anayekenua huyo mwenye suti ktk tukio hilo la taarifa ya Msiba huenda ana ugonjwa wa kucheka!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2013

    Huyo anyecheka uko nyuma ana ubinadamu kweli?ana roho ya nyoka huyo suti kama anaenda kuiba ming'oko vile

    ReplyDelete
  10. Dah! Yaani pole sana Dada Khadija. Nilisikitika sana niliposikia habari ya msiba wa mumeo. Yaani najua mlivyokuwa mnapenda. Mungu akutie nguvu dada. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2013

    UNA MAJONZI WANGINE WANAFURAHIA MAJONZI YAKO.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2013

    Hivi wadau mokoje? Mmemsikia jamaa akicheka? Kunonyesha meno au kufunua mdomo inawezekana anashangaa, analia, au labda kusikitika kwake ni kucheka. Remi Ongala aliimba "usione ninacheka, ukadhani ninayofuha moyoni...."! Msimlaumu baba sijui kaka wa watu. Kila mtu ana namna ya ku-react na certain circumstances! Na pengine hajui kinachoendelea! Yaani Wabongo ni lawama tu ndio maana hatufiki. Chukueni muda kutafakari

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2013

    Wakina baba Hawa wanatisha... Hata kutoa msaada kwa kina mama Hawa. Hiyo anaecheka hayawani tu.. Hata kama ni utani una muda wake, sio tu mara mfiwa anapotaarifiwa Msiba. Lakini pia, mpiga picha nae hovyo... Picha gani hiyo ku publish mtu yuko at the lowest point namna hiyo..

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2013

    Hawa waliomwambia nao hawakutumia akili si wangemwambia tu asitishe ziara yake mumewe mgonjwa sana na anahitajika mara moja Dar. Huko Rukwa sijui hata kama alipata usafiri wa ndege wa mara moja maana kendesha ni mpaka Dar ni siku nzima almost 18 hours? Sasa si kazi hiyo kwa mfiwa?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2013

    Pole sana msanii wetu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2013

    Pole Khadija Kopa. Jamaee hivi kufiwa afiwe mwingine ina maana life has to stop kwa wengine... je mnajuaje kama hata anajuana na kopa au ni msafiri yuko nazake??? Imetokea tuu bahati mbaya katokea kwenye picha anafurahia maisha yake na washikaji wake... dunia kila mtu na lake

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2013

    Huyu anaecheka anadhani atamuowa Khadija!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2013

    Pole sana Hadija naona hata pole haitoshi msiba usikie tu kwa wengine usiombe

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2013

    huyo anaecheka ana matatizo gani,tuwe tunajizuia jamani kwenye vitu kama hivi,mijitu mingine bwana

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2013

    Pole sana Hadija. Ila mumeo alikuwa anaumwa amelazwa, vipi uliweza kumuacha kitandani na wewe kwenda Namanyere? Huoni kwamba amekosa faraja kutoka kwako katika muda wake wa mwisho wa maisha. Any way yote ni mipango ya Mungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...