Mahmoud Ahmad,Arusha

Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo (CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo.

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi. Kamanda Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza tukio la bomu la kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo juzi.

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa wamukusanyana kwenye uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwepo uwanjani hapo akiwemo mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje na wabunge mbali mbali wa chama hicho walikuwa kwenye kikao cha bunge kinachoendelea hali hiyo imeliweka jiji hili kusimama shughuli zake kutokana na mabomu hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2013

    Chadema, acheni kutisha serikali! Eti, "mpaka kieleweke!" Hili ni tisho kwa serikali yetu. Kuweni waungwana; fuateni sheria ya nchi. Na endeleeni kuikosoa serikali kwa ustaarabu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2013

    Ngoja wagombea binafsi waruhusiwe kutakuwa hakuna cha CCM wala CHADEMA. Wananchi wamechoshwa na siasa za kitapeli. Polisi acheni kuwa branch ya CCM

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2013

    Wewe uliyetoa koment ya kwanza, wapi chadema iliacha kufuata sheria ya nchi? Unajua kilichotokea wewe Arusha? Au unakuja hapa kwenye blog kutoa matamshi yasiyo na uelevu, don't write something here if you don't know source from head to toe.

    ReplyDelete
  4. Mbona Majanga? nakumbuka kale ka wimbo ka Nusra;Ugomvi aanze yeye, polisi awahi yeye, kushikwa nishikwe mieeeeeeee!

    Polisi kuweni makini ipo siku ambayo Mungu tayari ameiandika mtapata aibu sana! Ni wazi mnajua kila kitu kinachoendela na acheni kutumiwa hata ktk issue za kuua!

    ReplyDelete
  5. Che GuevaraJune 19, 2013

    wewew anony wa kwanza ndio mwisho wako wa kufikiria?

    Ni nani ambae anawatishia wenzie? Polisi au wananchi? Hebu uwe unafikiria kidogo uchanganye na kaelimu kako kadogo kufikiria kabla ya kuandika lolote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 19, 2013

      Si unajua anapitia Lumumba baadae. Si kosa lake bali hali ngumu ya maisha. Majanga!

      Delete
  6. AnonymousJune 19, 2013

    KYALEMA! Ooops "CHADEMA"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2013

    tatizo kubwa ni Polisi kutoaminiwa na wananchi kutokana na mienendo yao na kutumiwa na chama tawala. Kwa mujibu wa Chadema polisi ni watuhumiwa namba moja ktk tukio hili sasa watafanyaje uchunguzi na tunategemea nini? ndio maana matukio yote yanayohusisha vyombo vya usalama, taarifa za uchunguzi bado hazijatolewa na haziwezi kutolewa kwa uhalisia. Mnakumbuka usanii wa taarifa ya Dr. Ulimboka?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2013

    mimi nadhani wote ambao mnamlaumu mchangiaji wa kwanza mpo kichadema zaidi kuliko uklwei halisi au upeo wenu ni finyu. hivi kweli ni sehemu gani duniani mahala kumetokea mlipuko kisha watu wakaruhusiwa kuweka kambi mahali hapo wakati uchunguzi wa tukio bado unaendelea? ila najua ndio upinzani wa bongo huo. sishangai siku mtakayoanza kujipinga wenyewe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2013

    tatizi ni kutokuelewa kuwa "HUWEZI KUISHI NA MWANAMKE/MUME USIEMTAKA AMA HAMUENDANI KITABIA" Pia michuzi kuwa na uhakika na unayoandika Mnyika hakuwepo alikuwa dar ila alikuwa anajiandaa kuja Arusha kujua yaliyowakuta viongozi wenzake jaribu kuficha hisia zako kwa kusema ukweli maana post za jana umeandika kuwa Nasari hajaumizwa kuwa dr anaemtibu kasema so pale hosp ni hotel ya kitalii kaenda kupumzika?????? hata usipopost umeisoma kimya kimya na umeelewa badilika

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2013

    Hii ni wazi kuwa polisi ni ka tawi ka ccm. Lukuvi anasema hiki, chagonja ansema hiki na yule kijana muenezi anasema kile kuhusu tukio.

    Hebu ona chagonja anapobadiri statement" Mbowe kumbe anajua wanaorusha mabomu halafu ananyamaza"

    Alishasema kuwa ni ffu ila labda hakuona sura zao alikuwa mbali , na ule mlipuko akili huwa inshindwa ku-concentrate.

    Sasa kitu cha kufanya hapa, Nnauye na Mbowe watoe ushahidi wote .Si chadema pekee.

    Mbowe alisema aliona FFU, Nnauye alisema ni Chadema.

    FFU na CHADEMA wote watuhumiwa .Ni bora Mbowe atoe ushahidi, na Nnauye kadhalika.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2013

    Nakumbuka kauli mbiu ya chadema ya kuhahakikisha nchi haitawaliki, nimeamini japo wanaoumia ni wanyonge maskini wa kufuata mkumbo. Acheni kupambana na polisi, nazi haiwezivunja jiwe. Tumieni nguvu ya hoja sio ya mawe, manatuharibia nchi yetu!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2013

    Jamani tunaelekea wapi wakati huu? Mbona mambo yamekuwa hivi mara mabomu ya mikutano ya dini na vyama. Usalama wa taifa upo au ulitangulia na mwalimu? Yaani threats za makaburu tulishinda leo ni nini kinatushinda kama upo? Kama kuna chama kinajihusisha na ugaidi huu wa kuuwa wapiga kura, sisi wananchi tutakifuta hicho chama na Mungu atusaidie. Acheni kutumia nguvu na vitisho vya kuuwa wananchi huo siyo ustaarabu hata kidogo. Matukio yanayolenga vyama vya upinzani yanatufanya tukichukie chama tawala CCM maana ni rahisi kuona ni hujuma ya wazi kwa upinzani kwa kuvitisha. Hakuna mpenda amani ataye chagua chama anachohisi kinatishia amani ya wanachi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2013

    ...kama eneo la tukio (viwanja vya Soweto) kwa maana hiyo bado uchunguzi ulikuwa unaendelea kama polisi walaivyosema ni sahihi kuzuia eneo hilo kuingiliwa maana kuna vitu vingi vya kusaidia upelelezi wa tukio.Polisi wako sahihi kwa hilo bila shaka yoyote...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...