MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Hiyo ni kinyume na maumbile, au?.....
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteInafurahisha na inachekesha kidogo. Lakini sababu twashangaa kuona mwanamke kuolewa na wanaume wawili ambapo hatuoni jambo mwanamme akioa wanawake wawili.Wadhungu wasema..what is sauce for the goose is sauce for the gander.
ReplyDeleteIncidentally I would appreciate if someone gave me tasir fasah ya msemo huo
Ibrahim
Kuna haja kuwaomba wanaharakati kushinikiza mfumo huu uwe rasmi. Kama wanapigania usawa wa kijinsia basi kila jinsia iwe na uhuru wa kuoa!!
ReplyDeleteOhooo!
ReplyDeleteHaya tena Mtoto wa Mkulima Mzee PM unatueleza nini kuhusu watu wako hao kwenye Jimbo lako?
Inafahamika ya kuwa sisi Watanzania ni jamii yenye kujinafasi sana hasa kwa mambo adimu kama hilo!, pana uwezekano mkubwa wakatokea Wanawake hapa Tanzania wakaupendelea utaratibu huo.
Je ikitokea Watanzania wakapendekeza Kikatiba KTK MCHAKATO WA KATIBA YA TANZANIA utaratibu huo Mtoto wa Mkulima unasemaje kuhusu hilo pia liingizwe kwenye Katiba?
Haya Baba Pinda kazi kwako unasemaje kwa hilo?
ReplyDeleteAhhh!
ReplyDeleteSio siri mambo haya wanaweza wanawake, inawezekana hao wanaume wanazichapa ngumi na kupigana vikumbo kwa siri, sio rahisi zamu ya mwenzio wewe ume umejikunyata pembeni.
Hiyo kwa wanaume inawezekana?
hilo ndio jembe, mipini miwili halali? mingapi mafichoni? ila watoto lazima watakuwa wanaumia kisaikolojia.
ReplyDeleteWanaume wawili mwanamke mmoja?
ReplyDeleteWanaume wanaweza hata kucheza mchezo wa Drafti au Bao kwa pamoja 'Dam dam' wakiwa nyumbani huku wakisubiri chakula!
Yote 9 la 10 ni pale chakula kimesha liwa...NA SASA NI ZAMU YA MWANAMUME MWENYE ZAMU YAKE SIKU HUYO KUJINAFASI!
OHHH HUYO MWANAMUME ATAKYEKUWA AMEAMURIWA KULALA CHINI YA MKEKA NA ''MWANAMKE-MUME'' MWENYE AMRI HAPO NDANI NADHANI PATAMBIMBIKA.
INAWEZEKANA HUYO MWENYE ZAMU ATAONGEZA MADOIDO HAPO KTK JUKWAA AKIJINAFASI HADI ALIYELALA CHINI KWENYE MKEKA NAYE AKAPANDISHA MORI NA KUKAIDI AMRI NAYE ILI 'APEWE' AKAPANDA JUU!!!
afadhali ana wawili wale machangudoa wana wangapi?
ReplyDeleteTwafa
ReplyDeleteINASIKITISHA SANA
ReplyDeleteHii ndoa ni halali? Ya kanisani (dhehebu gani)?, ya msikitini au ya Mwenyekiti wa Kijiji?
ReplyDeleteHongera sana Mama. Wewe ni shujaa wa mashujaa KuVunja Ukimya. Atakaye lima kando mpe talaka yake asonge mbali. Mdebedo, awe kipagazi kulima mashamba alite chakula kwa familia. Dunia Mbadala inawezekana!
ReplyDeleteWadau eleweni kwamba hatujajua kiini kikubwa cha hayo makubaliano,inawezakana kuna busara za hali ya juu kupita hata hizo haki za binadamu zinazoongelewa;Mfano,kama mume wa kwanza amepatwa na tatizo la JONGOo KUTOWEZA KUPANDA MTUNGI na ahadi ya ndoa yao ilikuwa kwa raha na shida,Lakini sio shida ya kukosa ngono.mume wa kwanza anaweza kukubaliana na mke ampate mtu wa kumtimizia shida yake ya ngono lakini huyo mume wa pili awe na wajibu mkubwa wakuitunza familia,inawezekana mume wa pili akawa kama mtumwa lakini kwamakubaliano!!AU mama huyu ni the main bread winner, anaweza kuwaambia ni kusuka au kunyoa.
ReplyDeleteHii ni busara, ni makubaliana ya watu. Kama anony mmoja alivyosema inawezakana mme wa kwanza jogoo hawiki. Na kama ni vinginevyo basi ni sawa na sisi tuwaowe, maana mmetuowa kwa karne nyingi muno. Asante Mheshimiwa Pinda kwa kibari hiki.
ReplyDeletehongereni wanawake kumbe na nyie mnaweza.
ReplyDelete