Na Enock Nyanda 
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sofia Mjema amesema manispaa ya Temeke inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa  vitendea kazi vya kuhakikisha hali ya usafi inaimalika katika wilaya hiyo.
 Mhe Mjema pia ameeleza kwamba Manispaa ya Temeke ni moja kati ya manispaa ambazo zipo mbele kabisa katika ukusanyaji wa mapato, ambapo ni wilaya pekee hapa Tanzania ambayo inakusanya kodi kwa wingi na kwa wakati muuafaka kutoka kwa walipa kodi wake. 
 Amesema swala la ukusanyaji wa taka ngumu limepewa kipaumbele hasa ukizingatia manispaa hiyo inazalisha ujazo wa tani 138,000 (elfu moja na therasini na nane elfu) kwa siku. 
"Tunaponunua vifaa kama hivi sasa tunahitaji kununua tena vfaa vingine ambavyo vitakuwa na uwezo wa kutenganisha takataka za chupa,taka ngumu na zile za karatasi. 
"Mkakati wa halmashauri ni kuongeza magari mengi zaidi ili kuweza kuendana na kasi ya kuwahudumia wananchi wake kwa kuhakikisha kwamba takataka zote zinazolewa kwa muda muafaka na haziachwi zikazagaa", alisisitiza Mhe. Mjema.
Naye Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo akitoa ripoti ya maendeleo ya usafi kwa mkuu wa wilaya alisema, halmashauri ya manispaa ya Temeke imeamua kununua magari matatu kuongeza ufanisi katika swala zima la ukusanyaji wa taka. 
Amesema Magari hayo yana thamani ya tsh.324 millioni ambayo yataongeza uvushaji wa taka ngumu kutoka 48% ambayo ni sawa na tani 455 kwa siku na kufikia 56% ambazo ni sawa na tani 515 kwa siku. 
 Ili kufanikisha zoezi hili manispaa pia imenunua magari mengine madogo yenye thamani ya tsh 102 millioni kwa ajili ya shughuri za usimamizi wa usafi,afya na mazingira hiyo yote ni katika kutekeleza maagizo ya mkuu wa mkoa wa dare s salaam ambaye aliwataka viongozi kushirikiana na watendaji wa kata na mtaa katika kuhakikisha wanaweka mazingira ya jiji kuwa safi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Photidas kagimbo akitoa ripoti ya maendeleo ya usafi kwa mkuu wa wilaya Bi Sophia Mjema (kati) kulia ni Meya wa manispaa ya temeke mhe. Maabad Suleimani Hoja
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe.Sophia Mjema akikata utepe kuzindua rasmi magari madogo mawili ambayo yamenunuliwa sambamba na magari ya kuondoshea taka ngumu katika manispaa ya Temeke
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Sophia mjema akizindua rasmi moja ya magari yaliyonunuliwa na manispaa ya temeke kwa shughuli ya uondoshashi wa taka,uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya manispaa ya temeke
Mkuu wa wilaya ya Temke Mhe Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati wa kuzindua magari ya uondoshaji taka katika manispaa ya Temeke

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jmani watz tubadirike. Uchafu sio kitu chema. Hasa dar es salaam kunatisha.

    Huko dar kuna mkusanyiko wa makabila mengi na hulka mbali mbali. Kuna wenye asili ya uchafu kuna wenye asili ya usafi pia.

    Temeke nawapongeza kwa hatua hiyo lakini je! wakazi wameelimishwa?
    Magari nayo yasije yakawa uchafu mwingine tena

    ReplyDelete
  2. Na hizo "PICK UPS" nazo zita beba taka?

    ReplyDelete
  3. Hata tuwe na Helikopta za kuzaolea TAKAKATA kama wananchi wenyewe hawana Ufahamu wa Usafi ni kazi bureee! Trust me leo nunua Dust bin weka mtaani utaona kama litajaa kwa siku mmoja? mtu anakunywa maji anatupa chupa chini, vocha sijui,machungwa mtu kala anatupa chini. kumbuka haya makari sio ya kuokota takataka ni yakubebea takataka. Nafikiri Elimu ya usafi na sherea za usafi zinatakiwa rekebishwa ndio mambo yataenda sawa. But it's good Idea kuwa na hayo magari ya kubebea takataka mazuri kuliko yale ambayo nayo ni takataka tunayoyaona every day. sijui anae wapa tenda wale jamaa wanao beba matakata yupo ulaya au ni kipofu au ya mjomba wake....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...