Jeshi la Magereza Tanzania Bara linapenda kuufahamisha Umma kwamba mnamo tarehe 23 Julai, 2013 Maafisa wanne ambao ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro, Sajenti Ketto Ramadhani, Koplo Silyvester Dionice na Wada Richard Barick wa Gereza Kiteto Mkoa wa Manyara walikamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la Jeshi la Magereza pamoja na silaha likiwa limepakia nyara za serikali. 

Dereva wa gari hilo Sajenti Ketto Ramadhan alitoroka na kutelekeza gari hilo na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na maadili ya Jeshi la Magereza pamoja na sheria za uwindaji wa wanyama pori. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Magereza limechukua hatua zifuatazo:-

i - Askari 3 waliohusika wamefukuzwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.

ii - Afisa Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro amefunguliwa mashtaka ya kinidhamu na kusimamishwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza hadi maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) itakapotoa maamuzi dhidi yake. Kwa sasa amezuiliwa Kituo cha Polisi Babati kusubiri kufikishwa Mahakamani upelelezi wa Polisi utakapokamilika.

iii - Mkuu wa Gereza Kiteto Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko kwa kutumia madaraka yake vibaya hivyo amevuliwa uongozi na kuhamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Manyara, akisubiri maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) kufuatia mashtaka ya kinidhamu yaliyofunguliwa dhidi yake.

Imetolewa na Kitengo cha Habari 
Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2013

    Doooohh Arusha/Manyara, FFU Bangi na mkoko wa POLISI , hawa nao Pembe na mkoko wa MAGEREZA kweli kazi ipo Nchini nani sasa atalinda usalama wa mwingine.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2013

    madawa ya kulevya.....

    vipusa, pembe za ndovu....

    nchi hii inaelekea wapi..!?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2013

    Ivi hile hukumu ya kuwahamishia wafanyakazi wahalifu toka eneo bora kwenda vijijini bado ipo?Kumbe ndio maana wakuu hawataki kuendeleza baadhi ya maeneo kwakua yanatumika kama adhabu kwa watendaji wahalifu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2013

    Haya ndo mapato ya uchumi m'baya wa nchi, unaweza kushangaa Afisa mratibu msaidizi wa magereza mzima anapata mshahara mdogo sana kulingana cheo chake, unadhani afanyeje sasa kujazilizia upungufu wa pesa hiyo.
    Ndo maana mimi nawaambia walipeni watu vizuri ili waheshimu kazi zao, mtu kama huyo kama angelipwa million 2.5 kwa mwezi badala ya 300,000/= (sijui kama hata zinafika huko), angeheshimu kazi na asingejihusisha na mambo ya kipumbavu hayo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2013

    Mfungaji kafungwa!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2013

    hiyo ni kaza za askari wa tanzania! by the way wanapewa ruhusa na wakuu wao; kwa mfano watu wakilete fujo wanaruhusiwa kuwapiga hata kuwauwa, mabomu wanaruhusiwa kutembea nayo na kulipua wanapotaka hata wakiuwa si kitu! Hizo pembe za ndovu na vingine vingi! Kwani miti inayokatwa msituni na kusafirishwa kisiri siri ni nani wanahusika! Bado kuna wapambanaji na rushwa lakini nao wanaogopa! Hata hawa waliokamatwa wale wanyonge watafukuza wengine wanahamishwa na kushushwa cheo! mambo ni yale yale!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2013

    Wengine nao wanajihusisha na uwindaji haramu tena wakitumia bunduki na gari la serikali,hivi tuna polisi au tuna wezi tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...