Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...