Hizi ni taswira za makovu ya vita baada ya  kuzuka vita Mwezi Oktoba 1978 ya Tanzania na nchi ya Uganda . Vita hii ilijulikana kwa jina maarufu la “vita ya Kagera” iliitwa jina hilo kutokana kwamba ilipiganiwa katika ardhi ya Tanzania mkoani Kagera. Vita hii ilisababishwa na kitendo cha Majeshi ya Uganda, chini ya Nduli Idd Amin Dada, kuvamia ardhi ya Tanzania katika eneo la Missenyi na kudai kuwa eneo lote lililo kaskazini mwa Mto Kagera ni ardhi ya nchi ya Uganda. Vita hivyo vilimalizika mwezi April, 1979 kwa Majeshi ya Tanzania kushinda vita na kumuondoa madarakani Nduli Idd Amin. Vita hivi vya Kagera vilikuwa na athari kubwa kwa mkoa wa Kagera. Athari hizo ni pamoja na vifo, wananchi kunyang'anywa mali zao na uharibifu wa miundombinu ya majengo na barabara.
 Taswira ya magofu ya lililokuwa kanisa la Missenyi ambalo majeshi ya Nduli Iddi Amin Dada yalibomoa kwa makombora na kuua ndugu zetu wengi  sana
Sehemu ya mto Kagera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2013

    Makovu mengine ambayo hayasemwi ni kwamba wanafunzi waliokuwa wanamaliza form 4 1978 shule za mjini ilibidi wakimbie shule kuoepuka mabomu na baadaye walipelekwa nje ya mkoa kwa ajili ya kufanya mitihani ya mwisho, muda huo wote wakati wenzao wa mikoa mingine wakifanya matayarisho wao hawakusoma na hapakuwa na consideration yoyote na matokeo yakawa mabaya!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013

    Ieleweke kwamba wakati vita hivyo vinapiganwa (na sio wakati vita hiyo inapiganwa) hakukuwa na mkoa ulioitwa Kagera, bali kulikuwa na mkoa wa Ziwa Magharibi, mpo wananchi?

    Mpiganaji kutoka Kishungambuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...