Kambi ya Wasanii wa Filamu na Maigizo pamoja na Kambi ya Waanahabari Makapela Tanzania imepata pigo kubwa baada ya Mwanachama wake Nguli, Simon Simalenga kuamua kuiaga kambi hiyo na kuingia rasmi katika Kambi Tawala ya Wanandoa baada ya kufunga Ndoa na Bi. Neema Inana. Wawili hao wameamua kuingia kambi hiyo ya Upinzani katika mahusiano leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza jijini Dar es Salaam na baadae katika tafrija kubwa inayofanyika usiku huu wa Julai 27, 2013 katika ukumbi qa Grande Hall uliopo ndani ya Hoteli ya Picolo Beach Mbezi. 
Production: MD Digital Company: +255 373 999/+255 717 002303 
Whatsapp +255 788 207274.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2013

    Utaratibu wa mbolea ya ruzuku umefeli. Kwa zaidi ya miaka 4 sijawahi kupata mbolea ya ruzuku lakini kuna majina ambayo hayakosi kupata mbolea hiyo katika kipindi hichohicho kwenye eneo ninaloishi huku Rungwe. Aidha ikifika inafika kimyakimya na "wahitajiwa na wahusika" fulani tu wanajulishwa. Alafu muda si mrefu baada ya mbolea ya ruzuku kugawiwa kwa "wakulima" tunaiona kwenye maduka kwa bei ya kawaida KK, Tukuyu mjini, Katumba, Mwankenja na kwingine. Wenyeviti wa vijiji na vitongoji wanahusika katika kuifanyia biashara mbolea iliyomlenga mkulima mdogo aongeze uzalishaji. Ni aibu kama serikali inadhani eti inamsaidia mkulima mdogo kwa mbolea ya ruzuku: inawasaidia viongozi na wafanyabiashara wachache tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...