Spika wa Bunge wa Bunge la Tanzania,Mhe Anne Makinda akihutubia kushukuru wajumbe Mkutano wa CPA Barani Afrika kwa kumchagua kuwa Rais wa CPA Afrika.
Mhe Spika Anne Makinda akipongezwa na Mwenyekiti wa CPA na Spika wa Bunge la Gauteng Mhe.Lindiwe Maseko,kwa kuchaguliwa na Mkutano huo wa 44 wa CPA kuwa Rais wa Afrika na Mwenyeji wa Mkutano wa 45 wa CPA utakaofanyika Arusha Tanzanis julai mwakani.
Picha ya pamoja ta Uongozi wa CPA Kanda ya Afrika, kutoka kushoto ni Mhe.Request Muntanga(Mweka Hazina),Mhe Asser Kapere ambae ni Rais aliemaliza muda wake na Spika wa Namibia,Mhe Lindiwe Maseko ambae ni Mwenyekiti na Spika wa Gauteng,Kutoka kulia ni Mr Demetrius Mgalami Naibu Katibu wa Kanda ya Afrika, Mhe Lucia Witbooi wa Namibia na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Afrika, Mhe Spika Sephiri Motanyane wa Lesotho na Mhe Spika Makinda wa Tanzania na Rais wa Afrika wa CPA.Picha na Saidi Yakubu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2013

    Hongera saana mama Makinda kweli una sifa zote za kuchaguliwa na uongozi wa CPA japo kutakuwepo na changamoto za vikwazo vingi,lakini umeshayakabiri mazito zaidi katika bunge letu tukufu la Tanzania sifikirii kama utakutana na jipya litakalo shindikana kupata ufumbuzi kila la kheri mama.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2013

    Hhahahahahaha dah!Lahaula, ama kweli..........usiku .........Haya si ya kuyafuarahia hata kidogo, huyu ni kama balozi sasa, anakwenda kuitangaza nchi, sasa hapa kuna mawili,1.kuitangaza vizuri nchi kwa kufanya kazi kwa umahili kwa kufuata kanuni na sheria(Kitu ambacho mara nyingi kilikua kikionekana kama kizito kwake).2.Kuvurunda na kuvipakazia vizazi vyote vitokavyo nchi hii(Kuiweka nchi ktk ramani ya majuha).Nina matumaini na utendaji mzuri huko kwakua, hapa alikua anabanwa na kundi maslahi.

    ReplyDelete
  3. AggripinaJuly 27, 2013

    Hongera sana Dada yetu; Role model wetu, rafiki Mh. Sp. Anne Makinda. Mungu na azidi kukupa busara.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2013

    Hongera mama makinda!
    Ingawa inachukuwa wageni kuweza kuthamini umahiri wa viongozi wetu na sisi wabongo huwa hatuchelei kushangiria na kuwaona wabora viongozi wanaopiga kelele na matusi. Udhaifu au mawazo duni tuliyonayo ni changamoto kwa Tanzania yetu.Mama Spika ni umahiri wako wa kuendesha shughuli za bunge kwa ufanisi ndio mwanga wa taifa. Hongera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...