Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na Haydom mkoani Manyara, walilazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, ambao baadae walilichoma moto basi hilo.
Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao wa vijiji vya Singa, Idabagadu. na Nkungi. mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.
Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita
Kwani lililoua ni basi au dereva aliyekuwa analiendesha? Elimu vijijini ni muhimu.
ReplyDeleteSasa wao wanadhani wamemkomoa mmiliki na siyo kampuni ya bima.
ReplyDeleteHawa wanakijiji sheria za nchi zipo na zifuatwe sio kujichukulia sheria mkononi hata kama mwenzao kagongwa na kufariki
ReplyDeleteChiki hizi ni zaidi ya mtu kugongwa tu! ina maana miaka tele tangia vijiji hivyo viwepo hakuwahi kufa mtu kwa kugongwa? Je walichoma gari husika pia?
ReplyDeleteHuu ni umaskini wa kupindukia, unaozalisha hasira kiasi hiki. Serikali ifanye kweli "Maisha bora kwa kila Mtanzania"