Katika mitandao hivi karibuni zilionekana picha za watanzania wawili waliovamiwa na kupigwa  vibaya  Ugiriki.
Picha hizo hazikuwa na maelezo ya kutosha  na hatimae zilizusha maswali mengi yaliyokosa majibu muwafaka.
Jumuiya ya watanzania ugiriki baada ya kikao cha tume maalum inapenda kutoa  taarifa kamili ifuatayo:
1.   Waliovamiwa ni Makamu Mwenyekiti  bw. SALUM MSELEM  na Mhazina bw. SAID MOHAMED SAID  maarufu kwa jina la NURAMO(CHIDI)  NDUGU HAWA SI WAKIMBIZI, NI WATANZANIA HALISI.
2.   Mabwana hao walikuwa wanapita kwenye garden usiku  wa Jumatano 01/08/2013 kuelekea makwao,wakitokea  kwenye kikao muhimu ofisini .      Karibu na  garden hiyo kulikuwa na wezi waliokuwa wanajaribu kuvunja gari iliyokuwa imeegeshwa.Wezi hao walijishuku kama Salum  kawagundua wakamfuata kwa vitisho na kuanza kumpiga. Wakati huo lilitokea kundi lao jingine la watu wasiopungua  kumi wakaanza kumkimbiza Chidi ambaye alijitahidi kukimbia hadi  kufika chini ya nyumba anayoishi Salum(umbali wa mita 50)  huku akipiga kelele na hapo waliendelea kumpiga.Kelele za Chidi kwa bahati zilisikika na mke wa Salum  ambae nae alipiga kelele za kuomba msaada zilizowafanya  wakimbie na kumwacha Chidi akiwa hoi.
3.   Ndugu zetu tuliwafikisha hospitali  na tulitoa ripoti polisi  wanaoendelea na uchunguzi ambao hadi wakati huu tunapoandika maelezo haya HAKUNA TAARIFA ZOZOTE CHANYA  ZA KUWAKAMATA WAHUSIKA.
4.   Uongozi wa jumuiya unashindwa kutamka  kuwa wezi hawa wana uhusiano na kile kikundi maarufu kinachochukia na kuwavamia  wageni.Hatuna ushahidi.Bali tuna imani kubwa walikuwa ni vibaka toka nchi jirani.
5.   Tumeamua kuutaarifu ubalozi na vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimetumiwa taarifa za awali za tukio hili.
6.    Mwisho jumuiya yetu inatangaza bila kusita:                                         VIONGOZI WETU HAWAKUFANYA BAYA LOLOTE  LILILOSABABISHA WAVAMIWE NA KUPIGWA. TUPO PAMOJA NAO KWA HALI NA MALI.
Ahsanteni                                                                            
                                                                                                     Kny
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
                                                                                              (Kayu Ligopora)  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kayu Ligopora !
    Kayu Ligopora !
    Kayu Ligopora !

    Na wenzako kwenye Kamati yenu.

    Hiyo Serekali ya Ugiriki inapumulia mashine ama ilikwisha fariki muda mrefu tu, hivyo haina tofauti na ilivyokuwa Somalia kipindi cha nyuma kidogo kwa miaka 20 iliyopita.

    Serikali inapozidiwa na Madeni (kama ilivyo kuwa Ugiriki sasa) inakuwa haina uwezo hata wa kununua Aspirini Moja ama hata uwezo wa kuehdesha Polisi Posti moja tu.

    Nawashauri ya nini tabu yote hiyo?, na kwa nini msiwasiliane na Mhe. Raisi Jakaya Kikwete mtumiwe ndege kurudi Nyumbani Tanzania?

    ReplyDelete
  2. Duhhh Ugiriki ni Ulaya au ni Afrika?

    Nchi imesha filisika kabisa yaani mpaka Mipango ya Ukabaji mnayo huko kama Keko na Manzese ???

    ReplyDelete
  3. Afadhali sasa tumeweza kuelewa.Na wewe unaetuandikia taarifa hii kwa nini usije bongo ukapata ulaji wako?maana nakuona umebobea katika kuyachambua mambo na kuyapanga.Mimi nimekuelewa kama vile nipo hapo ugiriki. Taarifa yako ni bab kubwa. Nakuhakikishia huwezi kukosa ulaji wako katika serikali au vyama. Usilaze damu

    ReplyDelete
  4. Poleni Wadau wa Uyunani. Hii taarifa yenu ina mapungufu mengi. Wezi kutoka nchi jirani wamewapiga WaTZ ambao ni Wakimbizi. Kwanini wasipige simu Polisi wakati wanakimbia nategemea kila mmoja alikuwa na simu ya mkononi? Pia polisi wa Ughaibuni wanafika sehemu ya tukio chini ya dakika tano. Pia Ughaibuni kila kona kuna Camera ambazo zinatizamwa na wafanyakazi na kama kuna tukio la uhalifu taarifa inapelekwa polisi mara moja na polisi wanaanza kuelekea kwenye tukio. Pia polisi wa Ughaibuni hutumia Helicopter kuwakimbiza wahalifu. Serikali ya Tanzania haihusiki na Mtz ambaye ameikimbia TZ na kuomba hifadhi ya kisiasa nchi nyengine. Ushauri wa bure 1)Nunue magari 2)Jaza form za wahanga wa uhalifu ili mpate kulipwa 3)Azisheni taasisi za "Minority" na kusaidiana na NGO za huko Uyunani ili kulinda usalama na maslahi ya "Minority" 4)Kwa wale waliokwisha pata uraia wa Uyunani wahamie UK, Germany, Holland, Belgium, Sweden, na Norway.

    ReplyDelete
  5. USHAURI WANGU:

    Huwezi kutatua suluhisho la kuumwa na njaa kwa kuchemsha maji ya moto na kunywa maji ya moto, suluhisho sahihi na la kudumu ni kutafuta chakula!

    Mdau wa No.4 suluhisho la kudumu ni alivyotoa Mdau wa No.1 nalo ni KURUDISHA MPIRA KWA 'KIPA' ambaye ni Tanzania One ktk Timu yetu ambayo kwa sasa yenye kuelekea kwenye mafanikio Kipa Mhe.JAKAYA MRISHO KIWKETE!

    Huko kooote mnapata tabu ya nini?

    Mtakapoomba tu ndege ile mnakanyaga Bongo nadhani Ndugu yetu Muungwana kabisa JK atawapatia mpango mpya wa maisha Tanzania mtaweza kwenda hata Gairo ama Magore Morogoro kuna Mabonde mazuri sana kwa Kilimo mtaweza kuunda huo Umoja anaosema Mdau mkiwa Tanzania na mkanufaika kwa Miradi ya Umoja na Kilimo ama uchimbaji Madoni hapa kwenu Tanzania.

    Yanini kwa wenyewe tena huko si itakuwa ni yale yale tu nchi za watu Belgium, Sweden na Norway?

    ReplyDelete
  6. Kayu Ligopora na KAMATI YAKO,

    Hivi mnatambua jinsi Serikali zinavyojiendesha?, bado mnasubiri ''Polisi ya Msibani Ugiriki'' ifanye kazi yake!

    Ndio kama Mdau wa kwanza anavyofafanua, nchi inapofilisika uwezo wa kununua Aspirini moja unayeyuka, achilia mbali ile kuendesha Polisi Posti hata moja ni wazi haupo, sasa ninyi mnasubiri POLISI YA SERIKALI ILIYO KWISHA FILISIKA (ambayo inawezekana wewe Kayu EURO zako ulizo weka akiba Kibindoni ni nyingi wakati hiyo Serikali haina hata EURO moja) NDIO IWAPE HUDUMA ZA KIRAIA KWA KUWASAKA WATUHUMIWA NA KAMA KUFUNGUA NA KUSIMAMIA MASHITAKA?

    ReplyDelete
  7. Jambo linguine nyie Watanzania Ugiriki achene ujasiri mbaya wa namna hiyo!

    Nyie ndio wale wanakubali kung'olewa meno kwa nyundo na tindo Vichochoroni huku wakijikaza kisabuni na wanapomaliz wanawa danganya wengine kuwa hawakupata maumivu.

    Pili, mmeonyesha dharau kwa kufanya majukumu ya Kiserikali wenyewe.

    Hizo si kazi za akina Mhe.Membe?

    ReplyDelete
  8. Moja kwa moja Kayu Ligopora ukitua nchini Tanzania utaungana na Mhe. Nape Nnauye ktk jukumu la Unezi wa Kisiasa ndani ya CCM!

    Kwa kweli wewe ni jasiri kama Jenerali Mohamed Sahaf wa Iraq ya Saddam Hussein na u mbishi ajabu na tumba unajua kizipiga!

    ReplyDelete
  9. Watoa maoni 1-8 nahisi hata shule mlikuwa mnapita nje tu,au ndio shule mwisho Darasa la Saba Tanganyika? si bora muende Zanzibar mwisho Form 2 kama ukifeli mtihani?

    Mtoa maoni wa Nne naona umebobea kuangalia filam za michezo ya kizungu ukaona kila kitu ni kweli camera,sijui helicopter sijui sim za mkononi,tafute shule uende dah sijategema kama Tanzania kuna watu wapumbavu kama hivi.

    Mwengine ati anasema mpira arudishiwe Keeper je huyo keeper anaweza kudaka? hao wachezaji waliokuwemo ndani wanatamani wawe substituted kisha unawambia wenzako warudi,

    Hata huko Bongo kuna kumwagiliana Acid,Kuna kuchubuliwa ngozi na pia kukata viuongo vya albino na kuuwana kila siku,tupisheni sie Muombeni nyie kwanza KIKWETE akupelekeni elimu ya Watu wazima angalau mpate kutoa ujinga.

    Mwengine ati Kazi za kina membe mnazifanya nyie ,ovyooo hajui hata nini maana ya jumuiya na diplomasia msijisemee tu taarifa imeeleza clear kabisa

    Kayu you have my support nyie mlotoa maoni hamjaombwa msaada mmeelezwaa tu nini kilichotokea wala habari haijaanza kuwa Tunaomba msaada, wala hamna mwenye shida na kuomba kazi ,ndio nyie kidumu chama cha mapinduzi kumbe mnakufa na njaa.

    Abdul UK Na Harudi mtuu nasubiri huyo atojibu sasa..

    ReplyDelete
  10. Abdul UK ''The East African' wewe tayari ni MKIMBIZI HUKO UINGEREZA NA NDIO MAANA UNAONA HATA AIBU KITWA MTANZANIA KWA KUWA SI MTANZANIA TENA NA SASA UNAZUGA KWA KUJIITA THE EAST AFRICAN !

    WEWE HUKO UK na WENZAKO AKINA KAYU LIGOPORA UGIRIKI MNATAKIWA MFUNGASHE VIRAGO MRUDI KWENU ''JAMHURI YA MUUNGANOM WA TANZANIA'' HUKO UK NA UGIRIKI MLIKUWA MMEOLEWA KWA NDOA YA MKEKA, HAO HAWAAMINIKI WANWWEZA KUUNDA SHERIA WAKAWANYANG'ANYA URAIA WENU HUO WA KIKIMBIZI NA BREKI YA KWANZA ABDUL UK ukajikuta upo KWA MTIPURA UNGUJA na KAYU LIGOPORA AKAJIKUTA KIJIJINI KWAO UBENA ZOMOZI MOROGORO!

    ReplyDelete
  11. Abdul UK 'The East African ni bora urudi kwenu Unguja ukavue samaki badala ya kuendelea kudhalilika UK kwa kuwa Kuli wa Kubeba Mabox.

    Kwa Heshima na Darja ya Ukoo wako Zenji ni fedheha kwa wewe kuwa Kuli Uingereza!

    Bora KAYU LIGOPORA yeye ni Bosi wa Jumuiya ya Watanzania huko Ugiriki.

    ReplyDelete
  12. Kuna wasioelimika wanatumia uwanja huu kutoa chuki zao za kibinasi na wala siyo kuongelea mada husika. Wapi na wapi kumshambulia Abdul UK na mada kuu iliyoandikwa na huyo KAYU?Inajionesha wazi kuwa huyu COWARD ANONYMOS anamjua vizuri Abdul na anamchukia kkwa maendeleo yake BUT THIS IS NOT THE PLACE TO EXPRESS PERSONAL ANGER

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...