Baadhi ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo.

===============
Mnamo tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.

Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.

Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.

Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3. JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. dani abdullahAugust 20, 2013

    mungu awape afueni nyote mliopata ajali.kwani taifa hili lina wategemea,mungu atawarudishen ktk hali njema,amin ila tu nimesikitishwa nahuyu muandishi aliyeandika habari hizi nizuri umeuhabarisha uma ajali iliyotekea lkn tu unakasoro ktk uhawandishi wk ningekuomba rudi tena chuo cha uandishi wa habar kwamba ujue hapa ni tanzania sio kenya au uganda hatuna ukabila wa udini hapa,hapa ni tanzania usileta ukabila mbona hukumalizia dini zao ;langu nihilo namimi kama nimekosea nakubali kusawazishwa,mimi ni mtanzania halisi jina daniel abdullah

    ReplyDelete
  2. Nashangaa sana polisi wanavyowataja watu na makabila yao. Nilidhani haya mambo ya kutajana makabila hatuna tena...kumbe yapo? Uendeshaji mbaya ni tatizo kubwa sana huko nyumbani, haingii kwenye akili ya mtu yeyote zaidi ya magari manne yahusike kwenye ajali kwa vipi? Kimsingi hata kitaratibu kote duniani magari hayatakiwi yafuatane kama magari ya mashindano. Magari yanatakiwa yaachane kwa umbali wa mita 30 iwapo yapo kwenye mwendo mkali.Mbona sharia za barabarani zinasomeka kirahisi hata suala la kutumia tu akili...Tatizo ni nini????

    ReplyDelete
  3. Haya mambo ya kuweka matuta hovyo ndio matokeo yake hayo. Kila wanapoona watu wanapita kwa kasi basi solition ni kuweka tuta! Huu ni ujinga kabisa, kwa nini msiweke speed limit na kuweka askari wakiwa na tochi na kuwapiga faini madereva wanaokiuka mwendo uliowekwa? Faini ni chanzo kizuri cha mapato kwa serikali badala yake wanakimbilia kutuwekea kodi za SIMCARD!!!

    ReplyDelete
  4. Mimi ni mtanzania sina chama lakini sasa hizi mbio za mwenge nafikiri mda umefika tuachane nazo! Kazi yake imeisha fanywa katika hiyo miaka 50 ya uhuru kumulika nchi japo haijawamulika mafisadi na mambo mengi yanayoendelea! Ni kupoteza pesa tu sasa!

    ReplyDelete
  5. Mh hamna mmakonde hata mmoja aliyekufa - lol

    ReplyDelete
  6. Gari No. T627BFJ Toyota Landcruiser Mali ya Chama cha Mapinduzi.

    Je, Chadema mbona gari lenu halipo ktk Msafara wa Mwenge?

    Ninyi Chadema sio Watanzania wenzetu?

    Kwani Chadema Mwenge sio suala la Kitaifa?

    Au na ninyi ni walewale na Jamhuri ya Rwanda na ninyi labda sio wenzetu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...