Taarifa kamili ya askari bandia wa Trafiki feki James Juma Hussein (45)  aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es Salaam ni hii hapa.
  Je, ni kwa nini 'Afande' James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye cheo cha ukaguzi (Inspekta) alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini. Alipomwona James alisimamisha gari. Akashuka kwenda kumsalimia. Lakini alipomkaribia alishangaa kuona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya polisi vinatakiwa kuandikwa "police force", akamtilia shaka.  

Baada ya machale kumcheza, afisa huyo alimkamata James Juma Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, Dar na kumfikisha kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari, wilayani Ilala, mkoa wa Dar es salaam, na kumfungulia jalada namba STK/RB/15305/2013 kwa tuhuma za KUJIFANYA ASKARI ili taratibu za kisheria zichukuliwe juu yake.
Mahojiano ndani ya kituo cha polisi yalikuwa hivi: 
Afande:Wewe mtu wa wapi?
James: Mnyamwezi, wa Tabora.
Afande: Una muda gani ukijifanya trafiki?
 James: Wiki moja sasa.
Afande: Hii kofia ya polisi uliipata wapi?
James: Nguo nyeupe juu ya kofia niliitengeneza kienyeji, krauni, tepe za usajenti na mkanda ni vya shemeji yangu. Alikuwa polisi mkoani Tabora, na sasa ni marehemu. Alikuwa akiitwa Shabani. James aliwaambia polisi kuwa suruali nyeupe ya kitrafiki aliishona mtaani lakini kamba ya filimbi na kizibao cha kung’ara vilikuwa vya polisi.
Askari: Uliwahi kuwa polisi?
James: Niliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) mwaka 1990-91 lakini nilifukuzwa kazi kwa sababu nilikwenda muziki. Nilirudi Tabora nikawa mkulima na mke wangu na mtoto mmoja ambao wote sasa ni marehemu.
Ndani ya nguo za kitrafiki alizokuwa amevaa James, alikutwa na suruali ya bluu na fulana ya kijani. James alisema njaa ndiyo iliyomfanya ajifanye trafiki na ‘kuwapiga mikono’ madereva, hasa wa daladala ili anapowakuta na makosa kwenye magari yao ajipatie chochote.
 Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa polisi huyo feki, ambaye atapandishwa kizimbani wakati wowote kuanzia sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Loo! maskini mzee wa watu. Mwonyetu tu jamani na kumwacha aendelee na maisha yake huko. Shida hizi kweli zinatufikisha pahala pasipostahili.

    ReplyDelete
  2. Mm najiuliza hiv? Hizi nguo alikua anazivalia wapi na kuzivulia wapi? Hata ulinzi shilikishi au majilani zake wasijue yote ayatendae,na kwa mtindo huu watakua wengi,chondechonde jamani wizara ya mambo ya ndani acheni utani fanyeni kazi zenu kimakini lasivyo hii nchi ipo siku itatekwa,pongezi kwa alie mgundua na pia mtoe mafunzo kwa raia wote ili wayajue majeshi yao vizuri hasa hasa kwenye uvaaji wao na alama zao,raia wakivijua hivi vitu inakua rahisi nao kumgundua MFEKI NA WA UKWELI,naitwa mdudu KAKAKUONA mwenye macho ma3

    ReplyDelete
  3. mimi naona bora aachiwe huru tu kwani wauwaji hapa nchini wako nje na mwenye njaa anafungwa sijui sheria mimi sikusoma shule lakini naelewa kuwa nchi hii ina matatizo.
    mdau.
    mlandizi.

    ReplyDelete
  4. JAMANI MIAKA 45 MTU UNAONEKANA KAMA UNAMIAKA 65?KAZI KWELI KWELI HII.

    ReplyDelete
  5. Mataruma says,
    Desperate measures for desperate people, bora ya huyu jamaa wangine wanafika hadi kutoa roho za watu. Tukiangalia kwa upana tatizo ni kwamba maendeleo ya nchi yanatengeneza tabaka za watu wengine kuwa juu sana na wengine kubakia chini sana; typical western style economy. Kama hali ya maendeleo ya uchumi haitorekebishwa (kupunguza gap) matokeo yake itafikia wakati kila mtu itabidi alale na bastola chini ya mto.

    ReplyDelete
  6. Mataruma says,
    Desperate measures for desperate people, bora ya huyu jamaa wangine wanafika hadi kutoa roho za watu. Tukiangalia kwa upana tatizo ni kwamba maendeleo ya nchi yanatengeneza tabaka za watu wengine kuwa juu sana na wengine kubakia chini sana; typical western style economy. Kama hali ya maendeleo ya uchumi haitorekebishwa (kupunguza gap) matokeo yake itafikia wakati kila mtu itabidi alale na bastola chini ya mto.

    ReplyDelete
  7. The guy was trying to get some money to go and buy food. The big fishes who are draining our monies through bad contracts are never touched, how unfair is that? Wake up bongoland!!

    ReplyDelete
  8. watu kama hawa wapo wengi jamani tuangalie sana polis feki wapo wengi sana wezi majambazi ndio hao hao jamani haya shida hizi mpaka zinamfikisha huko jamani

    ReplyDelete
  9. Hiyo ndo Bongo Daresalama

    ReplyDelete
  10. Masikini wa Mungu
    Tumuonee huruma.
    Angalia hata uso wake, its a picture of pure desperation.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  11. huyu jamaa anastahili tuzo na sio kuadhibiwa kwani amesaidia kuepusha ajali nyingi na watu kufuata sheria za barabarani

    huyu Jamaa amejitolea kufanya kazi bila kulipwa na ni volunteer wa nguvu inashangaza kumuadhibu

    Nimependa pale alipozongwa akajifanya kama kapoteza fahamu vile HI HIH IHIHI

    ReplyDelete
  12. I am happy the Fake police is caught. But if he seeks the real job government should send him for training. Secondly, We request to government to introduce special ID cards like the ones of Driving Licence which has the tin and record. When citizens are stopped they can demand to see their ID. This way even the fake ones will be caught...

    ReplyDelete
  13. Thought process
    What will stop the fake traffic obtaining a face ID card?

    ReplyDelete
  14. I have been thinking long and hard on how to assist this chap and i think he will do very well as an undercover reporter. Perhaps he can get professional training to add on to his skills. Hopefully he will disclose dodgy dealings etc. Au wampe kazi kwenye UN peace keeping in DRC/Mali/Libya ..n.k. As his calling in this life is about policing. Just a thought.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...