SERIKALI ya Ujerumani imetoa msaada wa Euro milioni nane (sawa na sh: bilioni 17.6) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi unaojihusisha na Utafiti wa kutambua mikakati bunifu ya kuimalisha usalama wa chakula kwa kutumia teknolojia na upelekaji wa maarifa kwa wakulima vijijini ( TRANS – SEC) katika Mkoa wa Dodoma na Morogoro.

Mradi wa utafiti huo wa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu na umelenga kuwajengea uwezo wakulima kwa kutumia utafiti shirikishi ambao utatoa fursa za utekelezaji wa malengo yatakayowanufaisha wakulima 4,000 kutoka vijiji viwili katika Wilaya ya Kilosa, Morogoro na vingine viwili vya Wilaya ya Chamwino , mkoani Dodoma.

Mratibu wa Mradi huo wa Trans – Sec nchini Tanzania, Dk Khamaldin Mutabazi, alisema hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti wa Mazao kutoka Idara ya Utafiti na Maendeleo ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika, Dk Hussein Mansoor , kuzindua rasmi mradi huo, Septemba 2, mwaka huu katika Hoteli ya Morogoro.

Uzinduzi huo pia uliwashirikisha baadhi ya watafiti mbalimbali kutoka Vyuo Vikuu vya nchini Ujerumani, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), pamoja na watendaji kutoka Mashirika ya Mitandao ya Wakulima nchini.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mradi huo , vijiji viwili vilivyoainishwa kutoka kwenye Wilaya hizo, vitafanyiwa utafiti wa kina wa kimazingira ya kijamii na kiuchumi yanayozunguka mifumo ya chakula ili kuibua mbinu bora za usalama wa chakula ikiwa ni pamoja na kutambua kiwango cha wastani cha mvua kwa mwaka.

Hata hivyo alisema , mbinu endelevu zitakazotumika zinasaidia kuleta mafanikio katika avijiji na mikoa husika na zitatumiwa kufikia walengwa wengi zaidi nchini na baada ya mradi kumalizika matokeo yataweza kutekelezwa katika ngazi tofauti za sera , ugani na utafiti.

Kwa upande wake , Mwakilishi wa Ubalozi wa Serikali ya Ujerumani hapa nchini, ( Head of Cooperation), Claudia Imwolde-Kraemer, alisema Tanzania ni nchi yenye historia ya utajiri wa rasilimali mbalimbali, lakini bado inakabiliwa na changamoto juu ya usalama wa chakula kinachozalishwa.

Hivyo alisema , Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Mendeleo ya kimataifa la nchi hiyo imeweka mkakati wa kusaidia kuzifanya rasilimali hizo zitumika kwa maendeleo ya wananchi wake.

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Ubalozi wa Serikali ya Ujerumani hapa nchini, Trans –SEC ,inafadhiliwa na Wizara mbalimbali za nchi ya Ujerumani ili kuwezesha watafifi kutoka Tanzania, Ujerumani, Kenya , USA na Brazil ili kufanya kazi kwa pamoja ya ufatifi wa miaka mitano .

Lengo ni kuwezesha kuongeza na kuimalisha usalama wa chakula kwa wakulima wadogo ambao hawajitoshelezi kwa chakula wanachozalisha kwa msimu pamoja na kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi duaniani .

Naye mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti wa Mazao kutoka Idara ya Utafiti na Maendeleo ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika, Dk Mansoor ,aliishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake hapa nchini kwa kuwezesha kuanzishwa kwa mradi huo muhimu wakati huu.

Hata hivyo alisema , wakulima wanakabiriwa na changamoto nyingi zinazohitajiwa kupatiwa ufumbuzi hasa ya uboreshaji mifumo ya miundombinu ya barabara, hifadhi ya mazao na uvunaji wa maji ya mvua ili yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza mavuno.

Mbali na hayo alisema A, mradi huo unakuwa ni chachu katika kuwezesha uboreshaji wa mazao ya chakula ili kukidhi haja ya kuwepo kwa usalama wa chakula nchini.
Meneja wa ZALF , Stefan Sieber ( kulia) akimpongeza , Claudia Imwolde-Kraemer ambaye ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania na pia ni Head of Cooperation wa Ubalozi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa na watatiti wakisikiliza moja ya mada iliyotolewa baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Trans - Sec
Watafiti wakishiriki katika uzinduzi wa mradi wa Trans - Sec

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wajerumani!

    Wajerumani!

    Wajerumani!

    Mmesikia mpya ya leo?,,,Vibarua wa Kampuni yenu ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi STRABARG Mishahara yao imeliwa na Vishoka!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...