Wema Sepetu akiwa na baba yake Balozi Isaac Sepetu siku alipotangazwa kuwa Miss Tanzania 2006. Kati ni mfadhili wa gari la zawadi alilopewa Wema kwa ushindi huo, Tanil Somaia
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii inaeleza kuwa Balozi Issac Abraham  Sepetu ambaye ni Baba mzazi wa Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu amefariki Dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinasema kuwa,Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.

Hadi Mauti yanamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam, jirani na hostel za Chuo Kikuu.

Globu ya Jamii inaungana na Waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Mwenye Kurehemu, Aiweke Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.

-Amen.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pole sana Wema. Mungu akupe nguvu. Tumwombee mzee Sepetu apumzike kwa amani

    ReplyDelete
  2. "INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN"

    WEMA silie jikaze, POLE sana dada yetu,
    MOLA umtangulize, ndo muweza kila kitu,
    KIFO hata tujibanze, khatima ya kila mtu,
    ILAHI PEMA MLAZE, ISAAC WA SEPETU.

    Mwenyeez Mungu amrahamu, amughufirie kwa yote na amlaze pahala pema Peponi - AMEEN.

    ReplyDelete
  3. poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  4. Poleni sana familia ya Balozi Isaac Sepetu pole sana Wema pamoja familia yote na dada na kaka zako wote. Pole my school Endita Sepetu. Rest in peace uncle Sepetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...