Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mh. Sadifa Juma Khamis akitoa Taarifa fupi kwenye Mkutano wa kutambulishana baadhi ya wajumbe wa Kamati ndogo ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu ya UVCCM Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu ya UVCCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, kulia yake Makamu Mwenyekiti wa Kamati Hiyo waziri Mkuu Mstaafu wa  Mh. Edward Lowasa pamoja na wajumbe wengine wakiwa katika mkutano wa mwanzo wa Kamati hiyo.
--------------------------------------
Wananchi wa Majimbo ya Donge, Kitope na Bumbwini yaliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” wameombwa kuitumia fursa na bahati waliyoipata ya uwepo wa kiwanda cha Sukari Mahonda ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nafasi za ajira wakati kitakapoanza rasmi kazi zake za uzalishaji wa sukari. 
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa salamu maalum kwenye Mkutano wa hadhara wa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Mkaratini ndani ya Jimbo lake la Kitope. 
Balozi Seif alisema tabia ya baadhi ya watu kujaribu kufanya hujuma kwa kuchoma moto mashamba yaliyooteshwa miwa ya kiwanda hicho inaweza kuwafukuzisha wawekezaji ambao tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyao hapa Nchini. 
Alieleza kwamba wananchi wa Majimbo hayo wanapaswa kuwa makini pamoja na kukemea vitendo hivyo viovu ambavyo endapo vitaachiliwa kuendelea kufanyika katika maeneo hayo vitachangia kurejesha nyuma juhudi za Serikali kuu za kukaribisha wawekezaji wanaopewa nafasi ya kuwekeza ili kusaidia uchumi wa taifa pamoja na ustawi wa jamii. 
“ Vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wenzetu tunapaswa kuelewa kwamba hatuwatendei haki wawekezaji wetu waliojitolea kuweka vitega uchumi vyao hapa Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.
Alisema inasikitisha kuona kuwa zaidi ya ekari kumi na nane zilizooteshwa miwa kwa ajili ya usagaji wa sukari wakati utakapoanza uzalishaji tunaarifiwa kwamba zimeteketea kwa moto unaosadikiwa kuwa ni hujuma za makusudi “. Alionyesha Masikitiko yake Balozi Seif. 
Aliwashauri wananchi hao kuwa walinzi wa miradi ya uwekezaji ambayo mingi kati yao huwanufaisha wananchi walioziunguukwa na miradi hiyo. Akizungumzia suala la siasa Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mbunge wa Kitope aliwatahadharisha wana CCM na wanachi wote Nchini kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wenye sera zisizotekelezeka. 
Alisema wanachokihitaji wananchi walio wengi nchini ni sera pamoja na kile wanachokihitaji kitekelezwe na Viongozi waliowachagua katika maeneo yao na si vyenginevyo. Alifahamisha kwamba baadhi ya wanasiasa hivi sasa wamekuwa kero mitaani kwa tabia yao ya kuendeleza matusi na lawama kiasi kwamba zinakwenda kinyume na mfumo wa vyama vingi vya siasa lakini hata na maadili ya dini. 
Aliwataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali yao yenye lengo la kuwaletea maendeleo kwa kujenga miundo mbinu itayotoa fursa ya kutanuka kwa huduma za Kiuchumi samba mba na kupunguza umaskini. “ Tunapaswa tuangalie kwa makini tokea mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hadi leo Bara bara ngapi zilizojengwa katika maeneo yetu. Sasa lazima tuelewe kwamba Zanzibar ni ya Wazanzibari wenyewe na wao ndio watakaohusika katika kuijenga “. Alisisitiza Balozi Seif. 
Aidha Balozi Seif alieleza kwamba lengo la Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Muungao kwa faida ya watu wake wote. Alifahamisha kwamba cheche ya ubaguzi inayoendelezwa na baadhi ya watu kwa kutaka kuvunja muungano haiwatendei haki Wazanzibari walio wengi wanaoishi upande wa Bara wa Muungano. Alisema choko choko hizo zinaendelea kuchochewa wakati tayari wazanzibari hao wameshawekeza miradi kadhaa ya kiuchumi inayoweza kusambaratika kama fitina hiyo ikiachiliwa kuchomoza zaidi. Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi alisisitiza na kuweka wazi kwamba msimamo wa Chama cha Mapinduzi uko wazi wa mfumo wa Serikali mbili ambazo ndio muhimili wa kuendelea kuwepo kwa Muungano uliopo hivi sasa. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 23/11/2013.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope.
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia matukio yaliyokuwepo kwenye Mkutano wa Hadhara wa Wana CCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo Kitope ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Haji Juma Haji.
Wana CCM walijikuta wakinengua wakati Kikundi cha burudani cha CCM Big Star kikifanya vitu vyake kwenye mkutano wa hadhara wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope. Picha na Hassan Issa wa OMPR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...