Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Singida. Dk. Mahenge amesema hayo akiwa anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Singida kukagua miradi ya maji katika Halmashauri za Wilaya ya mkoa huo.

“Nimetembelea mikoa karibu yote nchini kukagua miradi ya maji, lakini ni Singida pekee ambako karibu miradi yake yote imetekelezwa kwa asilimia kubwa, ikiwemo mitatu iliyokamilika na mingine ipo katika hatua nzuri kiutekelezaji”, alisema Dk. Mahenge.

“Nawapongeza sana watendaji Singida kwa kazi nzuri na nawashauri wasibweteke, bali wafanye bidii kuhakikisha mpaka mwezi Juni 2014 wawe wametekeleza mpango wa kutekeleza miradi yote na si vinginevyo”, aliongeza Dk. Mahenge.

Dk. Mahenge alifurahia utendaji kazi wa mkandarasi wa mradi wa maji wa kijiji cha Ng’unguli, kwa hatua iliyofikiwa licha ya kuwa na miezi mitatu tu tangu ianze na kuahidiwa kuwa mpaka mwezi ujao utakuwa umekamilika. Huku akisisitiza viongozi waelekeze nguvu katika miradi mingine itekelezwe kwa wakati na maji yapatikane.

Pia, alitembelea mradi wa maji wa Mamlaka ya Singida Mjini unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania, Badea na OFID na kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo mkubwa ambao unaendelea kujengwa na baada ya kukamilika utakuwa ni moja ya miradi mikubwa inayotoa huduma ya maji nchini.

Katika ziara hiyo Dk. Mahenge alifanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo Singida Mjini, Manyoni, Ikungi, Kiomboi, Puma, Iramba, Unghandi, Ikhanoda, Puma, Itigi, Iguguno, Nguvumali.

Mkoa wa Singida umepokea Sh. Bil 41.5 kwa robo ya kwanza ya mgao wa fedha mwaka 2013/14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya vijiji 10 na programu ya BRN.

Dk. Mahenge amemaliza ziara yake ya mikoa ya Dodoma na Singida mwishoni mwa wiki, katika kuhakikisha utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu ya wa Big Results Now na miradi yote ya maji inatekelezwa kwa kasi na ufanisi ili kuleta matokeo yaliyopangwa kwa wakati.
Naibu Waziri wa Maji,Mhe. Dk. Binilith Mahenge akipokea taarifa ya hali maji Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Naibu Waziri wa Maji,Mhe. Dk. Binilith Mahenge (katikati) akikagua mradi wa kijiji cha Nguvumali, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Dk. Binilith Mahenge akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Singida (SUWASA) hawapo pichani, kulia ni Meneja wa SUWASA Inj. Isaac Nyakonji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Dk. Binilith Mahenge, akisoma taarifa ya majumuisho ya ziara yake Mkoani Singida katika mkutano na viongozi na watendaji wa mkoa huo.
Mradi wa maji wa Mamlaka ya Maji Singida Mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Unajua nashindwa sana kuwaelewa watanzania sisi.Matatizo ambayo tunayo leo ya maji na umeme ni kutokana na mipangilio mibaya ya miundo mbinu na plan za jiji.Mtu anajenga nyumba kisha anaenda kuomba maji na umeme.Hii ni sawa unavaa suruali then unavaa chupi mwishoni kweli hii ni akili kweli?na hii wizara inakuwa inapoteza mali na fedha nyingi kutokana na kwamba hakuna upangliaji mzuri wa miundo mbinu na hii ni pamoja na tanesco.
    Pili,sijui kama wizara ya maji walishakaa na kufanya study kuhusu upotevu wa maji pili yanapokuwa yanatoka bomba kuuu na kuzambazwa.Mana ukienda kule mashenzini kule mabomba kibao yanavuja na hakuna mtu anayashughulikia,na kingine nathani kuna haja ya kuondokana na MA-SIMTANK.Iwekwe sheria itakayozuia kubeba maji zaidi unaytaka kutumia kwa siku na kuacha wengine wanshindwa kutumia,pia na matumiz ya mota kuvuta yale maji.

    Naamini hii wizara inataka mtu mwenye kichwa cha kutulia na upeo wa hali ya juu kuweza kutatua matatizo mengi ambayo yamekuwa yakiiusumbua hii nchi.

    Tatu,mamlaka za maji taka na maji safi pamoja na tanesco washirikiane na wizara ya ardhi na mipango jiji kuleta ufanisi na uboreshaji na hadhi za mazingira yetu.Mfano,kama nilivyosema hapo juu mtu anajenga tu,wizara ya ardhi imempa kibali ndio lakni je kuna mabomba ya chini kwa chini kwaa jili ya kuchukua au kukusanya sewages systems? pia hii inaweza kuwa kama kipato cha mamlaka husika.je maji masafi vip?na hali kathalika umeme pia.hii itasaidia kujua na kuwa na mpangilio mwema wa usambazaji wa maji safi na umeme pia.

    Suala la matank haya ya maji naomba waliangalie upya.
    Na hii ni kwa wizara nyingine tunaomba huko kwengineko kama mwanza na mikoa mingine mboreshe huduma zote na muwe na systems/infrastructures ambazo zinaeleweka.Sisi tunajua mnatoa madili ya uchimbaji visima huku huko chini ya ardhi kuna mtu anahifathi tank lake la maji taka basi maji yanapotembea chini huku baaala tupu.

    Ushauri wangu ni kwamba wizara ya maji ifutwe na iwe department ndogo chini ya wizara ya huduma kwa jamii ambapo mtu anweza kupata huduma zote sehemu moja kama maji safi maji taka,umeme,simu,internet na nk.

    na hayo maji machafu mnaweza kukusanya na kujenga kituo cha kuzalisha umeme ambao naami inawezekana.Sio kuchafua mazingira kwa kuwalisha samaki wetu maji machafu tu.Angalieni hata beach zetu ni chafu kwelikweli.

    MBISE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...