New Life Band ya Arusha
Lilian Kabaganza wa Rwanda

KUNDI la Muziki wa Injili la New Life Band la jijini Arusha limethibitisha kushiriki Tamasha la Krismas linalotarajia kuanza Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine minne hapa nchini.  
Bendi hiyo ni muendelezo wa waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo la Kimataifa lenye kauli Mbiu ya kuimalisha amani hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema kuendelea kujitokeza kwa waimbaji hao kunatokana na kufanyika kwa taratibu stahili ambazo zitafanikisha tamasha hilo.
“Bado tunaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine kutoka nchi mbalimbali ambazo ni majirani zetu, lengo ni kuimarisha uhusiano mwema na maendeleo mengine kwa ujumla,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema mbali ya bendi hiyo ya New Life Band, mwimbaji mwingine kutoka Rwanda ni Lilian Kabaganza.
Msama aliwataja wengine waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, kundi la The Voice (Tanzania), Solomon Mukubwa (Kenya).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani nimefurahi kuwaona New Life Band kwenye blog ya jamii. Namuona Madevu, Kaka Ondo na Baba Tina. Long time guys.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...