Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga, akisisitiza jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na ujumbe wa kampuni ya Symbion ya Marekani kujadili maandalizi ya ujenzi wa  kituo kikubwa cha maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), ambayo itashirikiana na Club ya Sunderland ya Uingereza katika kuindesha Academy hiyo. Katika mpango  huo, Kampuni ya Symbion pia itajenga viwanja vya michezo (sports courts) eneo la Kidongo Chekundu. Mazungumzo hayo yamehusisha pia ujumbe wa viongozi kutoka Idara ya Michezo (hawapo pichani)
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion, Ndugu. Peter Gathercole akifafanua jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuelezea mikakati ya Maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts).
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion, Ndugu. Peter Gathercole (kulia) akifafanua jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuelezea mikakati ya Maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni wajumbe alioongozana nao.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndugu. Leonard Thadeo (kushoto) akielezea jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, wakati uongozi wa Wizara ulipokutana na Ujumbe wa Viongozi wa kampuni ya  Symbion ya Marekani Kujadili Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Henry Lihaya  na Afisa Michezo Mkuu, Charles Yasse Mattoke. 
Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa  Kampuni ya Symbion ya Marekani walipokutana, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam kujadili maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). (Picha zote na Johary Kachwamba-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani mm naungana na nyie kuhusu huo mpango mzuri wa kimaendeleo,,lakini tujiulize je hiyo sehemu ni kubwa na inatosha ya kujenga hayo mambo mazuri? Mm naona tungelitanua jiji letu,tutoke nje ya jiji zaidi ili kupatikane eneo kubwa zaidi ya hapo,,naitwa mdudu kaka kuona,,nipo huku UINGEREZA

    ReplyDelete
  2. POLLUSION YOTE HIYO KATIKASTI YA JIJI HII INAONESHA NI JINSI GANI VIONGOZI WETU WASIVYO NA UPEO, KWANINI WASIENDELEZE KIJIJI CHA MICHEZO KILICHOTELEKEZWA KARIBU NA UWANJA WA TAIFA KILICHOPO BARABARA YA MANDELA? AMA KWELI SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...