Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu.
Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. CHURCH/MOSQUE AND STATE. MMMH I AM JUST PASSING BY.

    ReplyDelete
  2. waafrca tuna safari ndefu sana aise.mmh!!

    ReplyDelete
  3. usanii .com

    ReplyDelete
  4. Mambo ya Ajabu sana haya unaweza kuyaona Africa tu hususan Tanzania !!!

    ReplyDelete
  5. There is only one way. Jesus.
    No any other. l pray your spiritual eyes to be open people.

    ReplyDelete
  6. Hahahahaha ni nini na ni wapi kumbisale??????

    ReplyDelete
  7. Sala inaruhusiwa bwana anywhere...Hata ulaya they do the same, nimekaa ulaya sana and watu wengi tu wanakuwa wanaombewa kwenye sehemu zao za kazi, Obama mwenyewe first day kwa ofisi aliwekewa mikono. Sio useme hii africa tu ndio ipo your wrong. IN GOD WE TRUST. keep the spirit up. Binadamu kila kitu mnasema, Je angeleta mganga wa kienyeji hapo mngesema pia. khaaa hamuishi maneno? Bora huyu hata amewaleta mchana kweupee na picha hizi, hao wanakujaga Usiku na wanganga wao na kuvunja nazi? Big up Mh. heshimiwa, Ila unatakiwa kutubu tu ile Kauli yako ya kuwa WATANZANIA NI MASIKINI HATUWEZI KUVUNA MAFUTA, ukifuta ile Kauli utafanikiwa sana.

    ReplyDelete
  8. kama kawaida ya viongozi wetu, Huyu naye kaanza usanii. Nilidhani sio mwanasiasa kumbe ni walewale, umeme mgao kwa kwenda mbele na sababu kibao!

    ReplyDelete
  9. Hiyo Sala ielekezwe kwa Mwenyezi amkinge dhidi ya Nguvu moja hatari ya Ufisadi!

    Mhe. huyu ameshika dhamana kubwa sana nchini KAZI KUBWA ANAYO MBELE YAKE mwacheni kwa Mwenyezi aombe!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...