Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, akitoa utetezi wake, akidai kuwa ameonewa.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa amekutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe.  “Niliona nimtafute mkuu wa nchi (Rais Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge. Amekubali kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wao (mawaziri).”
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Akihitimisha mjadala huo wa ripoti ya kamati yake, Lembeli alisema: “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.”

 Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. kashiba ni haki yake aondoke,wanaishi maisha ya kifari kwa kuua tembo hata huruma hawana.amechuma zakutosha,tamu za watu si nzuri,hiyo tokomeza majangili iliishia kuuwa watu.na kuacha wahusika wakilala kwenye viyoyozi,hata ile deal ya wachina pengine mhusika mkubwa alikuwa huyo waziri,tunasubiri mizigo mingine ya nape aliyoisema

    ReplyDelete
  2. Duh! Hatimaye serikali imeanza kuamka kidogo katika kusikiliza malalamiko ya wananchi, nawapongeza Wabunge kwa kuacha tofauti zao za kisiasa na kuanza kuwashughulikia viongozi "MIZIGO". Naomba mambo haya isiwe nguvu ya soda.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  3. Kifo kwa tembo wa Tanzania oyeeee!

    Majangili wanachekelea na sisi tutaishia kulia.

    ReplyDelete
  4. haaaaa....!!! Spika Anne Msekwa??? Ankali umechapia..!!

    ReplyDelete
  5. Spika Mhe. Anne Msekwa!!. Bora umeelewa. Mtu akijikwaa hachekwi, unamezea tu kijana.

    ReplyDelete
  6. Mbona Hawa Ghasia ameachwa? Tungeambiwa pia utendaji mzuri wa mawaziri wengine kwani hata wizara zingine zina kero za siku nyingi tu.

    ReplyDelete
  7. Inapaswa washitakiwe hawa na sheria zifuatwe,japokuwa ni zaidi ya nusu ya mawaziri hawatufi, basi serikali onesheni mfano kwa hawa tuwaelewe kweli mmeamua kusimamia sheria

    ReplyDelete
  8. Haya ndiyo maamuzi magumu, idumu serikali ya CCM waliodhani kwamba haiwwezi kufanya maamuzi magumu kazi kwao

    ReplyDelete
  9. Mawaziri wanaoshighulikia tembo watimuliwa. Mawaziri wanaoshughulikia wanafunzi bado wanapeta. Hivi bunge letu tukufu linathamini tembo kuliko watoto wetu?

    ReplyDelete
  10. Jamani ili swala la acountability si dogo...hakuna nchi yeyote inaweza kuendelea kama viongozi hawajibiki au kuwajibishwa...

    Mnaweza sema hawa mawaziri hawajahusika moja kwa moja; lakini amini nawaambia sie watendaji wa chini tutakuwa na nidhamu kama wa juu watawekwa kiti moto. Wakubwa sasa hawata bweeka maofisini wakisubiri kuletewa ripoti; watawawajibisha vidagaa kablka ufagio hauawafyeka wao wenyewe...

    Bravo Bunge muendelee na moto huo huo uone ikifika 2030 kama Tz haitakuwa middle income country.

    Mimi namini kiongozi wa juu akiwa mkali hakuwezi kuwa na kashfa kwa watendaji wa chini...tokeni maofisini mchape kazi; si mnalipwa ela nzuri na magari ya fahari...ina maana walikuwa hawajuhi yanayotoka mpaka Bunge limeunda tume????

    ReplyDelete
  11. The mdudu K,anasema tunashukuru kwa hayo maamuzi magumu,,ila chonde chonde tokomeza MAJANGILI lazima iwe palepale ili tuwaokoe hao wanyama wetu,na hiyo tume itakapo undwa ikachunguze kiundani ili iwataje majangili wote waliohusika awe mweusi au mweupe lazima tuwafahamu,awe kigogo au wafanya bishara mapapa lazima tuwajue coz ni wahujumu wa taifa letu na uchumi wetu,tushachoka kuona wachache wakitwanga na kupeta kwa njia za mali za uuma huku wimbi la watanzania wakitaabika pasipo kufaidi mali zao za Taifa lao

    ReplyDelete
  12. MBONA MAGAZETI YAMESEMA WOTE WAMEPIGWA CHINI HAKUNA ALIYEJIUZURU.

    ReplyDelete
  13. Hongera sana wabunge.na huku kwetu znz wapo wengi hawa jamii ya akina kagasheki wanaotakiwa kuwajibika lkn hakuna hatua yeyote na serikali kimyaaaaa

    ReplyDelete
  14. Bunge letu kweli halieleweki. Yaani Mulugo na Kawambwa bado tu wanadunda pamoja na mkorogano na uozo wote uliopo wizara ya elimu!

    ReplyDelete
  15. Ibara 37 kipengele cha 3 cha katiba kinamzuia Rais kufanya maamuzi yeyote akiwa nje ya nchi , badala yake makamu wa Rais ndiye anatakiwa kutoa Executive Orders. Na yeye kama hayupo PM anatakiwa kutoa orders. Vipi waziri mkuu apige simu kwa Rais na kupokea orders?????? katiba imekiukwa . Sefue fafanua hili kabla upinzani haujaamka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mh hii haijakaa vizuri na PM si mwanasheria?

      Delete
  16. Pamoja na kasoro zilizojitokeza katika operesheni TOKOMEZA za raia na askari kuuwawa, niukweli usiopingika wanamtandao wa UJANGILI nchini wameshinda vita kwakuwatumia wabunge ili wao wasiguswe tena, nakudhoofisha kabisa jitihada zakulinda hata hao TEMBO wachache waliobakia.Wanyama hawa am so pia no urithi was Dunia wamekosa watetezi kwasababu2 hawawezi kupiga kula ndio sababu zilizotolewa bungeni, mungu a2saidie sana.

    ReplyDelete
  17. Kuwadhibiti Tembo na wanyama Pori:

    Ni wakati sasa huku tukishirikiana na Ujerumani tulioingia nao Mkataba karibuni na UNESCO inatakiwa tuwafunge wanyama ELECTRONIC BADGES ili kuweza kuwaona KIDIJITALI muda wote pamoja na wanaowazunguka kama ni Majangili na kuweza kufuatilia ni nani atawadhuru ni vile itaonekana live!

    Bila ya njia hii ya KISASA NA KIDIJITALI watafukuzwa wengi hata aje Nabii kuwa Waziri wa Wizara hiyo ya Maliasili ni wazi itafikia wakati atalaumiwa na atang'oka!

    ReplyDelete
  18. Hivi Khawawezi kupiga kula!!!!!! ndio nini

    ReplyDelete
  19. Mbona mmemshika Kawambwa. Hii wizara tokea enzi za Prof. Malima iliamdamwa hivi hivi wakikaa watu wa aina yake. KULIKONI. Haya na Hawa Ghasia ameshasema uozo ameukuta. Sisi tunaofanya kazi serikalini tunajua watu walioko chini ikiwa hawakupendi watakufanyia kila aina ya visa na ndio hao hao kutoka North. Mali asili wakurugenzi na maafisa wa Maliasili ndio walaji wakubwa wanajua kila pembe ya msitu na wanyama na nani yuko kusaidia biashara na kama hakutekeleza kazi aliyotumwa hana kazi au atakufa. Wizara zote zina watu walioko muda mrefu pale ambao ni wanandugu kwa sababu wamepeana kazi wenyewe kwa wenyewe na operations zote na projects za wizara wanazijua. Akiingia Swai basi angalia maafisa walioko chini yake. Akina Mapunda sio sana Lakini kina Nshomile nao wanaongoza kwa kuweka mtandao wa watu wao. Tena this is a fact. Si tunawaona tunafanya kazi nao na kila siku wanaajiriwa haohao. Siku hizi wengine waomba kazi tayari wameshaambizana waondoe majina ya ukoo katika vyeti vyao ili asijulikane kabila. Kwa hivyo jina ni Ester Michael basi but they are the same people. Waziri akipewa kuongoza wizara afanye nini. Labda kuwe na spoils system. Get rid of all of them and employ new ones? SIASA NAYO IKO WIZARANI. SISI TULIOKO TUNAIONA.

    ReplyDelete
  20. Waziri wa Maji naye aondoke, nchi haina maji halafu wengne wapo busy na biashara ya maji kny magari, wanayatoa wapi? Mbona mabombani kwetu hayatoki? Au maye ana ubia? Bomba la kuleta maji toka Ruvu ni lile lile tangu enzi za mkoloni, sasa waziri gani analala tu hawezi hata kubuni miradi mipya na kuitekeleza? Waziri wa MAZINGIRA NAYE aondoke maana hii nchi ni chafu hasa mijini, misitu inateketea, halafu mawaziri wapo tu wamekaa tu ofsn. Shame on them

    ReplyDelete
  21. mawaziri wa nishati na maji pia 100% wang'oke maana hakuna jipya wala nafuu kwa wananchi maji yamekuwa tatizo la kuduu miaka nenda rudi kama alivyosema mdau hapo juu. Na ukja huko kwenye nishati ukosefu wa umeme umekuwa tatizo kubwa sana. Au ndio chanzo cha kukuza biashara ya majenereta na solar za vigogo?

    ReplyDelete
  22. "....Siku hizi wengine waomba kazi tayari wameshaambizana waondoe majina ya ukoo katika vyeti vyao ili asijulikane kabila. Kwa hivyo jina ni Ester Michael basi but they are the same people....."WEWE MDAU ULIYEANDIKA HIYO COMMENT KAMA NI KWELI BASI NI HATARI KUBWA HUKO MAOFISINI KWENU.

    ReplyDelete
  23. Ningemsifu sana Rais, na kumuona ni mtu wakuchukua maamuzi magumu kama angemuondoa waziri wa TAMISEMI.

    Vile vile kama angewaondoa wafuatao mara moja.
    1. Wakuu wote wa wilaya ambapo haya yametokea.
    2. Wakurugenzi wato wa wilaya hizi
    3. Wakuu wote wa mikoa hii.
    4. RPCs wa mikoa hii
    5. OCDs wa wilaya hizi

    Hapa ndiyo tutakuwa tunafanya mabadiliko ya kweli. Otherwise huu ni utani.

    ReplyDelete
  24. kazi nzuri bunge la 14

    ReplyDelete
  25. Tutabadili mawaziri hadi tutachoka, tatizo ni mfumo wa serikali umekaa hovyo. Waziri wa elimu hawezi kumwajibisha mwalimu au afisaelimu wilaya au mkoa kwani Wako chini ya tamisemi. Waziri wa ardhi hawezi kumwajibisha afisa aridhi wa wilaya wala kumwamisha kwani Yuko chini ya tamisemi. Waziri wa afya hana mamlaka kwa mganga mkuu wa wilaya kwani hayupo chini yake. Mambo yapo hivi kwa wizara ya mambo ya ndani kwani ma OCD wanawajibika kwa IGP na ndiye anaweza wahamisha au wafukuza kazi n.k. Kwa hiyo wizara zinabaki kua za bajeti tu na mawaziri wanabaki kua wa bajeti tu. Kwa mtindo huu waziri hana nguvu yoyote. Huu mfumo lazima ubadilike tuwe na wizara chache ili wizara zingine ziwe idara ndani ya wizara kama tunataka mawaziri wafanye kazi zao vizuri

    ReplyDelete
  26. Mm namuunga mkono mdau anaezungumzia wizara ya maji. Tatizo la maji limekuwa sugu. Wafanyakazi wa DAWASCO ni kero namba 1 kwa wananchi. Mm ni mkazi wa Tegeta. Hebu nenda DAWASCO ofisi za bunju ukaone jinsi wananchi wanavyonyanyasika. Kuna mtu anaitwa Yasin na Damson. Hawa jamaa wangeondolewa ili kupunguza kero. Sidhani kama wamewahi kusikia kitu kinachoitwa 'huduma kwa wateja'. Halafu si manager wala waziri anaefatilia kero za wananchi. Kuna baadhi ya maeneo hasa tegeta utakuta mabomba ya maji yamekatwa na hivyo kusababisha njia zisipitike. DAWASCO wanadai watakuja kurekebisha. Je waziri ana tambua tatizo hili?? Mdau tegeta

    ReplyDelete
  27. Kweli kabisa madai ya mdau wa tegeta. DAQASCO wana tabia ya kunyanyasa wateja. Wateja hao hao wanalipa bili kwa huduma ambazo hawapati. Eneo la tegeta lina julikana kama malishio na bwawa la wanyama. Hili linatokana na mambomba yaliyokatwa kwa visu vikali. Serikali za mitaa wanatambua tatizo hili sugu ambalo limedumu kwa miaka kadhaa. Mitaa inalazimika kufungwa kutokana na madimbwi ambayo yanaletwa na mambomba yaliyokatwa. Huyo engineer kazi yqke kutoa ahadi hewa kuwa tutarekebisha mfumo mzima wa mabomba. Mpaka leo hii hakuna kilichofanyika. Ma manager wa bunju hawaishi kubadilishwa. Hii inaleta usumbufu. Kwani kila manager mpya anataka mteja arudie historia ya matatizo yake. DAWASCO BUNJU NI KERO NAMBA 1. TUNAOMBA MSAADA.

    ReplyDelete
  28. Wanatakiwa wapigwe bakora 6 hadhalani

    ReplyDelete
  29. Chinja wote hawa.
    1. Wakuu wote wa wilaya ambapo haya yametokea.
    2. Wakurugenzi wato wa wilaya hizi
    3. Wakuu wote wa mikoa hii.
    4. RPCs wa mikoa hii
    5. OCDs wa wilaya hizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...