Ankal akimkabidhi zawadi ya Krismasi  na kadi Kamanda wa FFU Ughaibuni The Ngoma Africa Band ya Ujeruman, Ras Ephraim Makunja, a.k.a Field Marshal wa jamii ya Annunaki walipokutana leo katikati ya jiji la Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya faragha ya saa moja katika kiota cha Break Point cha mjini. Katika mazungumzo yao waliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza undugu uliopo baina ya Globu ya Jamii na FFU Ughaibuni, na kupanga tarehe ambazo The Ngoma Africa Band itakuwa huru kuja kufanya maonesho kadhaa nchini Tanzania.
 Ras Makunja anarivenji kwa kumkabidhi Ankal zawadi ya moja ta T-Shirt kibao alizomletea zikiwa na logo ya Globu ya Jamii.
 Ankal akimshukuru Ras Makunja kwa zawadi hiyo mwanana
Ras Makunja akiwa na mjomba wake akijiondoa eneo la tukio taratibu huku kakumbatia zawadi yake ya Krismasi na kadi. Meno yote arobaini yako nje kwani hakutegemea kupata heshima hii. Picha kwa hisanio ya mpiga picha wa The Ngoma Africa Band aliyeongozana naye katika ziara hii ya mapumziko jijini Dar es salaam. Mara ya mwisho kufika Bongo kwa Ras Makunja ilikuwa miaka sita iliyopita, na ameshangazwa na mabadiliko na maendeleo makubwa aliyotaona kila mahali, kuanzia nyumbani kwake mtaa wa Aggrey ambako mbavu za mbwa yao imeshajengwa bonge la Ghorofa, nusura apotee, na huko kwake Segerea ambako anasema kuna lami mpaka jikoni....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ras Makunjaz Karibu sana Nyumbani !!!

    je (kiumbe) Bundi umekuja naye?

    ReplyDelete
  2. Kwao ilikuwa sio Aggrey ni Mtaa wa Mchikichi.

    ReplyDelete
  3. mkuu wa kazi Ras makunja vipi Bundi wako umekuja nae au?

    ReplyDelete
  4. jamani kamanda Ras makunja tunakuomba tukusikie live linunagani au redio?

    ReplyDelete
  5. Mkuu wa kazi,mmiliki wa himaya kuu ya viumbe wa ajabu Anunnaki,meja jeneral,Field Marshal,Afande wa kikosi maalumu ughaibuni,Karibu sana
    Tanzania

    ReplyDelete
  6. mjamaa anaitwa Ebrahim Makunja siyo Ephrahim,kiumbe wa ajabu anayefuga midudu ya kutisha

    ReplyDelete
  7. sasa kamanda lini? tutakusikia ukijojiwa live redioni,wadau tungefurahi sana kusikia mahojiano

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...