Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari  hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar.

Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Mwili huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.

Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala.

Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Loohh!Watanzania wenzangu tufanye kazi halali kwa bidii,tuache mambo ya njia za mkato.Hapa tulipofikia sasa sipo.Sitaki kuingilia kazi za kiupelelezi za polisi lakini hawa wanaodakwa na madawa ya kulevya,nyara za serikali(ujangili) nadhani kuna haja ya kuwa wanapigwa picha na wanawekwa hadharani ili watanzania wawaone.Hii ya "kuihifadhi" majina ndiyo imetufikisha hapa tulipo.

    David V

    ReplyDelete
  2. inashangaza majina ya wahalifu kuhifadhiwa ina maana wasijulikane,na makachero watajadiliana vipi nini cha kufanya ina maana hawajui wafanye nini na maiti na hao watu waliowakamata na madawa?comment zangu huwa hazitolewi naamini blog authour amesoma huu ujumbe anyway

    ReplyDelete
  3. Wadau hapo juu Zingatieni points hizi:

    1. Kutoa majina yao mapema kunaharibu upelelezi.

    2. Kama mhusika ana uhusiano na bosi wa aliyemkamata, usitarajie atajwe.

    ReplyDelete
  4. Naungana na Mkubwa hapo juu Ndugu David V.

    Watanzania tunazo Fursa nyingi sana za kutafuta Maisha na tukapata vipato vya halali kuliko Kazi hizi za GET RICH OR GO TO PRISON LIFE SETNTENCE OR DIE !!!

    Kwanza ni aibu kubwa ikijulikana ya kuwa mtu umefanikiwa kimaisha kwa kazi ama biashara za uhalifu kama hii.

    FURSA LUKUKI ZILIZOPO TANZANIA:

    SEKTA RASMI:
    1-KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA.
    2-UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NA MIFUGO MINGINE KAMA NG'OMBE NA MBUZI.
    3-UCHIMBAJI WA MADINI
    4-USINDIKAJI WA MAZAO YA VYAKULA.
    5-UTAYARISHAJI WA MADINI.
    6-UFUGAJI WA NYUKI.
    7-UKATAJI MAGOGO NA MBAO.

    SEKTA ZISIZO RASMI:
    1-UGANGA WA KIENYEJI KWA LESENI.
    2-USANII WA KOMEDI KWENYE MABAA.
    3-UANDAAJI WA LISHE BABA NTILIE NA MAMA NTILIE.
    (UCHOMAJI CHIPSI, VIAZI, MAHINDI ,MIHOGO NA MISHIKAKI,UUZAJI SUPU, UCHOMAJI VITUMBUA NA UKAANGAJI MAADNAZI NA CHAPATI VIKIWEMO NDANI)

    MAFANIKIO BILA BIASHARA YA UNGA INAWEZEKANA,

    TANZANIA BILA BIASHARA YA UNGA PIA INAWEZEKANA!!!

    ReplyDelete
  5. Hahahahaha Mdau wa 4 hapo juu hizo Fursa ni zaidi ya Bingo!

    Kazi kwetu Utajiri tunao mikononi ila hatujui nafasi hizi.

    Wengi wa wanao fanya kazi za Uhalifu pamoja na kama hizi hujiona wao ni wajanja sana, lakini mwishowe wanakuja kujuta wakiwa chini ya Mikono ya Dola.

    Tatizo wengi ni Mabishoo kazi kama hizo wanaona ni za chini wakati wao wakiwa ni Wajanja wa Mujini na Mapedeshee Jijini Darisalama!

    ReplyDelete
  6. Wadau mmetoa hoja za msingi. Ajira Tanzania sio unga tu. Lakini kumbukeni watanzania wanapenda njia za mkato. Utajiri wa harakaharaka kwa kazi kidogo, utajiri bila jasho. Uvivu wa kufikiri na kutenda unalitesa taifa.

    ReplyDelete
  7. Tatizo lingine pale Kariakoo watu Wafanya Biashara wengi wanaishi kwa Mashindano ya mafanikio na kulazimisha Malengo ya kimaisha.

    Watu wanashindana Ujenzi wa Maghorofa hadi kufikia kujenga chini ya viwango na Maghorofa kuporomoka kila uchao!

    Wanacho tazama wao ni urefu na ukubwa wa jingo tu, bora Punda afe lakini mzigo ufike.

    Sasa kwa Mashindano hayo ya KUTAFUTA FEDHA si ndio watu wanafikia kusafirisha maiti na kuibebesha Madawa ya Kulevya?

    ReplyDelete
  8. Hii kasi ya kutafuta Utajiri balaa!

    Marehemu Dr.Remi Ongala aliimba Wimbo huu:

    JAMANI DUNIA EEE, JAMA DUNIA, KABURI LA MWENZIO WAJENGA NYUMBA, ETI UMEPATA KIWANJA HUJUI KUFA WEWE!

    Na ndio hawa Jamaa wafanya Biashara ya Unga wanavyo ifanya maiti ya mwenzao kama Kontena la kusafirishia Unga wakiwa na wao ni waja watakao kufa kama alivyo kufa huyo maiti!

    ReplyDelete
  9. Mawazo pevu

    ReplyDelete
  10. Kila anayeweza kutumia ujanja kupata pesa ajaribu. Atakae kamatwa au kufa atajiju!!

    ReplyDelete
  11. Si-ajabu tena Tanzania kwa ujinga na laana kama hizi. Hapa ndipo nchi ilipofikishwa, laana kwenda mbele Rushwa na kutowajibika, kesi hii itaishia kinyemelaa kama nyenginezo ziliowahipita.

    Ikiwa binaadamu aliyemfu amtumiliwa hivi,bilashaka hata wanyama na nyama pamja na bidha nyengine zinazosafirishwa zinatendewa hivihivi.

    Zindukaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...