Mbio za kuwania ubunge katika Jimbo la Kalenga unabaki kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kuthibitisha kutosimamisha mgombea.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Abdul Kambaya, amesema chama chake hakina mpango wa kusimamisha mgombea katika jimbo hilo na kwamba hivi sasa wanaandaa mikutano ya kuimarisha chama chao.
“Mpaka sasa CUF haina mpango wa kusimamisha mgombea ubunge Kalenga… kwa sasa tunaandaa kikao cha Kamati Tendaji kitakachokaa kati ya Februari 15 na 16 mwaka huu ili kujadili masuala mbalimbali,” alisema Kambaya.
CHADEMA imepanga kumtangaza mgombea wa kiti hicho wakati wowote baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kuketi mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuteua jina la mgombea.
“Kwa sasa chama kinakusanya fomu za waliojitokeza kugombea jimbo hilo… hadi sasa tunaendelea na zoezi hilo, mwamuzi wa mwisho ni kamati kuu itakayoketi mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya uteuzi wa jina hilo,” alisema Ofisa Habari wa Chama hicho, Tumaini Makene.
Juzi CCM ilimtangaza Godfrey Mgimwa, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha na Uchumi, marehemu  William Mgimwa, kugombea katika uchaguzi mdogo, ambao kampeni zake zitaanza rasmi Februari 19, mwaka huu.
Mgimwa alichaguliwa kwa kura 348 za maoni za wajumbe 708 kati ya wajumbe halali 816 wa CCM katika mkutano mkuu wa jimbo hilo, na aliibuka kidedea kati ya wagombea tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. CUF ilikuwa chama kikuu cha upinzani ila leo hii katika chaguzi ndogo zaidi ya ishirini zilizofanywa wiki iliopita hatujawasikia kabisa. Sidhani kama mkiwa na timu ileile iliyokiangusha chama kufikia hapo mlipo mtaweza kukijenga chama tena, uroho wa madaraka umewaponza.

    ReplyDelete
  2. CCM mbona hehind the scene wako wazee walewale, jaribu kuchunguza utaona. Na wana ushawishi mkubwa sana. Na ukienda kwenye CHADEMA nako ni hivo hivo, walioko juu wanaweza kuwa ni wasemaji, behind the scene wako wenyewe. Kwa hiyo as long as viongozi wanapatikana kwa taratibu walizojiwekea waendelee. Nafikiri mdau hapo juu nikifikiri unataka kusema kwamba viongozi wa CUF walioko madarakani wamevunja sheria ili kuwa madarakani, lakini umesema tu kwamba VIONGOZI WAMEKAA MADARAKANI MUDA MREFU. Hiyo siyo hoja.

    Utoe ufumbuzi nini CUF wafanye ili waweze kuwa na wawakilishi zaidi? Huenda wazo lake litasaidia, kuhusu viongozi hilo halina tatizo kwani wanapatikana kupitia taratibu zilopo. OTHERWISE KUTAWEPO CHAOS AMBAYO SI NZURI NA NI HATARI KWA NCHI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...