Kutoka kushoto ni mratibu mwenza wa Tamasha la Jogging, Mashauri, Mratibu wa Jogging, KP, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mratibu wa Matukio wa Global, Luqman Maloto na Meneja wa Stamina, Said Ramadhani 'Kabwela'.
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Msoondo Ngoma, Said Mabela akizungumzia maandalizi yao katika bonanza hilo.

Mambo yameiva! Waratibu wa lile tamasha kubwa la mbio za taratibu (jogging) na huduma ya habari mpya zilizotokea punde ya Global Breaking News chini ya Global Publishers wameahidi kufanya makubwa ndani ya Dar Live Jumapili hii.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza ya Afrika-Sana, Dar leo asubuhi, meneja mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kuwa shughuli itakuwa nzito hivyo watu wafurike kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake.

“Baada ya jogging, kutakuwa na burudani kubwa ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa, Nay wa Mitego, Stamina, H. Baba na bendi inayopendwa na wengi ya Msondo,” alisema Abby Cool huku akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza Dar Live itaangusha burudani ya nguvu bila kiingilio.

Kwa upande wake, mratibu wa tamasha hilo la jogging, KP amesema: “Jogging itaanzia pale Uwanja wa Taifa hadi Dar Live. Vikundi zaidi ya 150 vimethibitisha kushiriki. Watu waje kwa wingi kuona mambo matamu bure kabisa kwani hakutakuwa na kiingilio.”

Naye meneja wa msanii Stamina, Kabwela aliahidi kuwa Stamina amejipanga kufunika vibaya siku hiyo kwani amekuwa kwenye mazoezi ya kufa mtu.

Mbali na Jogging, Breaking News, pia Global Publishers imetambulisha shindano lake jipya la Global Star Search litakaloanza hivi karibuni kwa lengo la kuibua vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
PICHA HABARI NA ERICK EVARIST/GPL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...