Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi (Kushoto) akipata maelezo
mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi
Mramba wakati wa Halfa ya kupokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme yenye thamani ya Dola za
Kimarekani milioni 183 itakayokwenda kufungwa Kinyerezi ambapo mitambo hiyo itaanza kufanya kazi
mwezi wa kumi mwaka huu.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi akishuka
kutoka juu ya meli wakati wa Hafla ya kupokea mitambo miwili ya kuzalishia umeme thamani ya Dola
za Kimarekani milioni 183 kutoka kwenye Kampuni ya General Electronics ya Marekani inayokwenda
kufungwa Kinyerezi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya mitambo ya kuzalishia umeme ikipakiwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda
Kinyerezi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa Tatu na kukamilika mwezi
wa kumi mwaka huu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) ambapo mitambo hiyo
imepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi. (Picha zote na
Benjamin Sawe wa Maelezo).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...