Kijana wa kitanzania asomae Korea Kusini Bw. Sunday Sokoni ameibuka kidedea kwa kushinda nafasi ya pili katika mashindano ya kukariri na kuongea mashairi ya kikorea kwa hisia. 
Shindano hilo liliwakutanisha washindani mia moja na therethini (130) wengi wao wakiwa ni Wakorea lakini Sunday Sokoni alifanikiwa kuwabwaga Wakorea hao na kuwa raia pekee wa kigeni aliyeingia kwenye Tatu bora. 
 Ushindi wa Sunday ulikuwa gumzo jijini Seoul-Korea na kupelekea Television za Korea kufanya mahojiano na Sunday Sokoni na pia kutengeneza documentary zinazoelezea maisha yake Korea amabapo ilimfaya kuwa maarufu sana hapo Chuoni (Yonsei). 
 Habari za Sunday pili zilishapishwa katika magazeti kadhaa ya kikorea pia alisikika mpaka katika redio mbalimbali za Korea. Tayari Kijana Sunday ameshafanya mahojiano kwenye television kadhaa; Chosun Tv na KTV na kwa sasa anajiandaa kuenda katika television kubwa maarufu iitwayo KBS (Korean Broadcasting System) kwa mahojiano anatarajia kufanya mwaka huu 2014 March na bado anaendelea kutafutwa na stesheni za television kwa mahojiano, kwa sababu imekua ni historia kutokea mtu wa kigeni kushinda mashindano hayo. 
Amekua ni kijana pekee ambaye kwa ujasiri wake na kujiamini kwa nafasi hiyo aliweza kupeperusha bendera ya Tanzania na kufanya nchi yetu itambulike zaidi hapa Korea Kusini. Sunday Sokoni ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Yonsei akisomea shahada ya Uchumi.
Sunday Sokoni akiwa amepozi katika moja ya picha zilizochapishwa kwenye gazeti la kikorea (Yonhap News)
Sunday Sokoni akipokea medali kutoka kwa mkuu wa chuo cha Yongsei Bw. Kap-Young Jeong baada ya kutangazwa mshindi wa pili wa shindano la kuimba kwa hisia mashairi ya kikorea
Pichani: Bwana Sunday Sokoni akihojiwa na television ya Korea( Chosun Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera kijana kaza buti kotekote ktk shahada yako ya Uchumi na pia Lugha ya kigeni. Maana vyote ni muhimu.

    ReplyDelete
  2. Bab kubwa Sunday....peperusha bendera kivyovyote vile.Lengo ni kujenga hesima...na kufukia mashimo yanayochimbwa na wengi tena usiku na mchana wakiwemo punda.....

    ReplyDelete
  3. Respect kwako braza Sunday.... Keep t up

    ReplyDelete
  4. Wa-Tanzania tunakuja tena kwa moyo safi.

    Sunday.. HONGERA SAANA !!
    hukuiwacha Nchi kila ulipooneka kwenye mkono wako.

    Kidogo kidogo Tutafika tu.

    ReplyDelete
  5. Asanteni sanaaaa Watanzania wenzangu huko nyumbani
    Si tutazidi kuwawakilisha vilivyo kokote tuwapo.Peace.Peace

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Sunday. endelea kuwakilisha.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Suday.

    ReplyDelete
  8. hongera sana sunday,ulionyesha mwanzo mzuri tokea tuko pamoja pale shule ya msingi mfaranyaki mjini songea,hongera sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...