Hiki ni kikombe cha chai ambacho kwa Tanzania bara kilichomo hutwa chai ya rangi ama chai ya mkandaa. Kwa Zanzibar ni Chai kavu... Yaani ukiagiza chai ya rangi uwapo visiwani unaletewa ya maziwa. Upo hapo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mie nakanusha kabisa! Hiyo siyo kweli kwa mujibu wa ulivyokizungumzia hicho kikombe cha chai, khususan CHAI KAVU kwa upande wa Zanzibar.

    Nnavyofahamu mie, Zanzibar (Unguja na Pemba) kuna Chai za aina mbili, Chai ya RANGI na Chai ya Maziwa. Ispokuwa ukitaka hiyo CHAI KAVU uloizungumzia ndivyo sivyo, kwa Zanzibar unaletewa Chai tupu! Yaani isiyokuwa na Kitafunwa/kitafunio chochote, si mkate, andazi wala manda, barka ya Chai kavu tu, baaaaaaaas! Na haijalishi kama ya RANGI au ya MAZIWA. Almuradi kikombe cha Chai tu, kikiwa na chai yake ndani, isiyokuwa na kitu chochote cha kusindikizia, mathalan mkate, muhogo, kiazi, n.k.

    Nadhani muhusika wa hicho Kikombe Cha Chai, ungefanya tafiti zako kwa kina na ufasaha zaidi, ndipo ungeweza kukinadi na kukielezea vizuiri hicho kikombe cha Chai na khasa hiyo chai kavu kwa upande wa Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. Mleta mada unahakika na ukichoandika!? Sijui unazungumzia Zanzibar ipi? Ila kwa Zanzibar mimayoijua Mimi chai ya rangi huitwa hivo hivo au wengine hutumia chai kavu na vile vile kwa chai ya maziwa huitwa hivo hivo chai ya maziwa na sio kama ulivosema chai ya rangi ndio ya maziwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...