Hapa Marikiti mjini Zanzibar ndipo kilipokuwepo kituo cha daladala mjini Unguja, Hivi sasa kimeshahamishwa na kuachwa kweupe na raha mustarehe kwa wakazi wa visiwani
Raha mustarehe kwa wana Unguja
Zogo sasa limehamia Michenzani karibu na afisi kuu za CCM za Kisiwandui ambako daladala zote husimama kwa sasa. Hakika kuna haja kubwa ya kuliangalia swala hili..Maana hapa pahala pafinyu mno!
Nadhani pale pale darajani (Marikiti/Market) ndio palipokuwa panafaa na palistahili kuwa kituo cha madaladala kama hapo awali, kwanza eneo lile ni kubwa ambalo lilikuwa na uwezo wa ku-accommodate takriban daladala nyingini na ziendazo sehemu mbali mabli, isitoshe kiusalama wa raia wendao kwa miguu japo haukuwa salama zaidi, ila sio sawa na hapo MIchenzani ambapo barabara kwanza finyu, pia msongamano wa watu, isitoshe kuna skuli/shule hapo pembeni Kiswanduwi (Kisiwanduwi), imagine wanafunzi wanapotoka shule si ndio hatari zaidi, mana huyu kakatisha hapa huyu pale, huyu anakimbilia daladala hii, huyu ile, almuradi tafrani na ghasia tupu. Sina hakika kama 'Risk assessment' has been taken, before arriving to that resolution. Labda kama kuna 'udhuru' wowote pale Marikiti uliopelekea kituo hicho kiwe hapo Michenzani. Pengine ni kwa muda, lakini kama ndio kimefika, basi Serikali itabidi iliangalie kwa ukaribu zaidi suala hili, kwa kuzingatia zaidi suala zima la usalama barabarani kwa abiria na vyombo vyao, wanafunzi wendao na kurudi mashuleni, kadhalika na wote wendao kwa miguu kwa jumla, mbali ya waendesha baskeli na marikwama. Mnazimmoja pia the same issue, labda kama itakuwa ni ule ule utaratibu wa daladala kwenda kuteremsha wale wendao huspitali hapo hapo kupakia wanaorudi na kugeuza, ila kama ndio kimefanywa kituo khasa cha kusubiri kwa muda mrefu kama ilivyokuwa Marikiti, basi pia itabidi serikali iliangalie jambo hili na ku-find alternatives.
ReplyDelete