Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama (liesimama) akitoa muongozo wa namna vikao vitakavyokuwa vinaendelea kufanyika katika kumbi mbali mbali ndani ya Hoteli ya Malaika,iliwa ni muendelezo wa Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa,unaoendelea kufanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Wengine pichani toka kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo,Mh. Everist Ndikilo,Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Charles Kitwanga pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza.Picha na Othman Michuzi,Mwanza.
Mwenyekiti wa Kikao kinachojadili maswala ya Ufugaji katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mh. Said Magalula na Kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Bw. Fanuel Lukwaro
Mtoa Mada iliyohusu Fursa za Uwekezaji katika Ufugaji na Michakato ya kuwa na Machinjio bora,Prof. Lazaro Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (Idara ya Sayansi ya Wanyama) akisisitija jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA,Dkt. Adelhelm Meru akifafanua jambo wakati akielezea namna EPZA inavyofanya kazi kwa wawekezaji mbali mbali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. Everist Ndikilo akifatilia kwa makini kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...