Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,lililomalizika leo kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Mh. Chiza amelifunga Kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ambaye hakuweza kuhudhulia kutokana na kubanwa na shughuli nyingi za Kitaifa.Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa siku tatu mfululizo,liliweza kujadili mambo mengi kuhusiana na fursa ya kuwekeza katika Kanda hiyo ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kufunga Kongamano hilo lililokuwa likifanyika kwa siku tatu katika Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Chifu Paschal Mabiti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini,Julieth Kairuki akitoa taarifa ya Kituo chake na jinsi wanavyoshirikiana kikamilifu na Wawekezaji mbali mbali wakiwemo wa ndani ya nchi na wale wanaotoka nje ya nchi.ambapo amesema kuwa Kongamano hilo limekuwa ni kama ishara ya uzinduzi wa mkakati endelevu wa kuibua na kunadi fursa mbalimbali zilizopo katika kanda ya ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Ally Rufunga akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wakuu wenzake wa Mikoa ya Kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Mara,Kagera na Geita.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo akiwahoji wajumbe wa Kongamano hilo kuhusiana na kuwepo kwa Mwenyekiti wa Kongamano hilo,ambaye ni Mh. George Kahama (kulia),ambapo Wajumbe wamempokea vyema Mh. Kahama na kusema kuwa anafaa kabisa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa Kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...