Sidhani kama vijana wa umri chini ya miaka 37 watajua hili, ila kwa wenye umri zaidi ya huo watakumbuka mabasi ya East African Railways maarufu kama mabasi ya 'Relwe' ndiyo yaliyokuwa kinara wa usafiri ini na Afrika Mashariki ya Kenya, Uganda na Tanzania kabla ya kuvunjika  kwa jumuiya hiyo mara ya kwanza mwaka 1977. Kabla ya hapo nchi hizo zilikuwa na shirika moja la ndege, meli, usafiri wa barabara na reli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mie nayakumbuka sana,inaonyesha umri wangu. Katika safari moja kutoka Dodoma kwenda Korogwe nilikuwa na saa ya mfukoni ya hayati baba, njiani nikafanya urafiki na vijana wa shule fulani na wakaanza kunifundisha wimbo "Show me the way to go home" na nini maana yake. Tulipofika Korogwe saa ya mzee imetoroshwa kutoka mfukoni kwangu.

    ReplyDelete
  2. .Jeshi letu la polisi bado wanayo mabasi ya muundo huu.Pongezi sana Jeshi la polisi.Kanda ta ziwa kulikuwa na Lake Tours(Lekitwaazi).Bila kusahau ze KAMATA

    David V

    ReplyDelete
  3. Inanikumbusha mbali sana, masikini. Lakini katika ujanja wangu wote sijaweza kuelewa maana ya RAB kwenye hiyo sahani ya namba. Mwenye kufahamu naomba msaada kwenye tuta, tafadhali.

    ReplyDelete
  4. Haya yalikua na first class.

    ReplyDelete
  5. Those good old days. I remember travelling to Dar from Mbeya with mum for our annual holiday. We used to sit in the first class compartment ... Just behind the driver... i can still sense the smell of ndizi's. Tukifika Iringa the bus went for service/refueling whilst me and other passengers waited in the freezing cold outside the station as the waiting room was packed. If the bus broke down, there was always a replacement bus came to the rescue. The speed was excellent. I cannot recall accidents. Thank you ndugu michuzi for taking the likes of me down memory lane. Hopefully the powers above can have a transport museum which will have these Railway buses, Dmt, UDA, Ikarus n.k trains too on display, so that our children and generations to come can view them and keep the history kinda alive.

    ReplyDelete
  6. RAB - Railway Authority Bus

    ReplyDelete
  7. Kumbwe wengi ni vijana wa siku hizi hizi! Nilikuwa darasa la pili Malkia elizabeth II anatawazwa - enzi za Mkoloni!

    ReplyDelete
  8. Nashukuru na ninasema kwa majivuno kuwa mimi niliwahi kuitumikia Jumuia ya Afrika Mashariki kupitia Shirika la Posta na Simu (EAP&T) mkoa wa Tanzania kama fundi katika karakana zake Dar es salaam. Baada ya kujiendeleza kielimu nilikwenda nchi za nje kwa masomo ya juu. Utalaamu na elimu niliyoipata vilinisaidia kuwa mtu muhimu sana katika kampuni ya Ericsson Sweden nilipokuwa nikifanya kazi zaidi ya miaka ishirini. Nashukuru kuwa ni mmoja wa watalaamu tulioshiriki katika kuianzisha GSM (2G) hadi WDMA (3G). Katika yote hayo kulikuwepo mkono wangu kama Mtanzania. Mungu Ibariki Tanzania.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...