Arsene Wenger jana alipatwa na majanga mawili ya mwaka baada ya kula mweleka muda mfupi baada ya timu yake ya Arsenal kupigwa 5-1 na Liverpool. 
Meneja huyo wa washika bunduki wa Uingereza alikuwa anawahi treni kurudi London katika mtaa wa Lime jijini Liverpool akiwa na wachezaji wake alipoteleza na kuanguka pwa! 
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 64 anaokenana pichani akiwa anaburuta begi lake wakati akiingia stesheni, lakini mara tu baada ya kuvuka mlango wa kuingilia, anateleza na kula mweleka. 

Mfaransa huyo aligumia kwa maumivu wakati askari polisi wawili walipofika kumsaidia. Msemaji wa Arsenal alinukuriwa baadaye akisema kuwa mzee mzima hakuumia na hajambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Pole masikini, sifikiri kama wenye nyumba walikuwa wapo, maana akili zake zote zilikuwa
    zafikiri, hivi kichapo hiki ni kweli ama ni ndoto tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...