Mhe. Hussein
Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akifungua mafunzo hayo rasmi
jana, katika maneno yake ya ufunguzi Kattanga amewaasa Makarani kutokufanya
kazi kwa mazoea bali kufanya kulingana na misingi ya maadili ya Mahakama
iliyopo lengo likiwa ni kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi, (kushoto) ni
Msajili wa Mahakama ya Ardhi, Mhe. Lameck Mlacha, kulia ni Naibu Mkurugenzi
Mafunzo, Bi. Rehema Vyas.
Mmoja wa Makarani kutoka
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipendekeza jambo mbele ya Mtendaji Mkuu kuhusiana
na maboresho ya huduma ya utoaji haki kwa wananchi.
Baadhi ya Makarani
wa Mahakama wakiwa katika Mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Learnit
kilichopo jijini Dar es Salaam.
1.
Mhe. Hussein
Kattanga akiwa darasani kushuhudia baadhi ya wanafunzi hao wakipewa somo
kuhusiana na mfumo wa kuingiza taarifa za mashauri/kesi kwa kutumia kompyuta,
aliye pembeni na Mtendaji huyo ni Bw. Machumu Essaba, Mkuu wa Kitengo cha ICT,
Mahakama ya Tanzania, na wengine waliosimama kwa nyuma ni baadhi wa wakufunzi
wa Mafunzo hayo ambao pia ni Watumishi wa Mahakama, Kitengo cha ICT.
Mtendaji
akiendelea kushudia wanafunzi wakiwa katika mafunzo hayo. Lengo la Mahakama ni
kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki nchini inapatikana kwa urahisi kwa
kutumia njia za teknolojia hususani katika kuingiza taarifa muhimu za kesi kwa
kutumia kompyuta. Mafunzo hayo ambayo yatachukua jumla ya siku 21 yanajumuisha
jumla ya Makarani 30 kwa kila wiki, ambapo kundi la kwanza litamaliza mafunzo
yake siku ya Jumapili 02.03.2014.
Mgeni rasmi
aliyefungua mafunzo hayo ya Makarani, Mhe. Hussein A. Kattanga, Mtendaji Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania (katikati), Mhe. Lameck Mlacha, Msajili wa Mahakama ya
Ardhi (kushoto), pamoja na Bi. Rehema Vyas, Naibu Mkurugunzi Mafunzo, Mahakama
ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi (Makarani) wanaohudhuria
katika mafunzo hayo na baadhi ya Wakufunzi wa mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...