Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imekuwa ikikutana na wanahabari katika
kuandaa utabiri wa msimu ili kupata michango yao na kuifanyia kazi kadri
inavyowezekana kwa lengo la kuhakikisha taarifa sahihi zinatolewa kwa wakati
muafaka.
Baada ya kukutana na wanahabari hao katika warsha zaidi ya tatu ikiwemo ile ya
lugha itumikayo katika kutoa utabiri wa msimu, TMA imeona ni wakati muafaka
sasa kwa Mamlaka kuweza kupata mrejesho ili kuweza kuboresha ushirikiano
wake na vyombo vya habari katika kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa jamii
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alisema
anavishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano ambao umewezesha
taarifa za tahadhari ya hali mbaya ya hewa kuifikia jamii kwa wakati muafaka.
Alisisitiza kwamba kikao hicho ni cha muhimu kwani pamoja na mambo mengine
kitajadili changamoto wanazokutana nazo wanahabari katika kufikisha taarifa
za utabiri kwa walengwa.Dkt Kijazi aliongezea kwa kusema kikao hicho kitatoa
mapendekezo ambayo yataiwezesha Mamlaka kuboresha namna ambavyo
taarifa za hali ya hewa zinafungashwa (packaging) ili wanahabari wazielewe na
hivyo kuwafikia walengwa zikiwa sahihi na kwa wakati.
Aliwaambia wanahabari
wawe huru wakati wowote kuulizia jambo lolote linalohusu hali ya hewa ili
kupata ufafanuzi utakao wawezesha kutoa taarifa sahihi
Mshiriki kutoka TBC1 Bi. Mwasu Sware akizungumza kwa niaba ya wanahabari
amesema hivi sasa mamlaka ya hali ya hewa imejitahidi sana kuwa karibu na
vyombo vya habari na hivyo kuzifanya taarifa za TMA kuwafikia wananchi kwa
wakati.
Lakini pia TMA inatakiwa kutumia lugha rahisi na nyepesi ambayo haina
misamiati mingi ya kisayansi ili kuwasaidia waaandishi kuelewa na hivyo
kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Alisema ipo haja pia kwa TMA kuwa na task team[ waandishi maalumu] ambao
watakuwa karibu zaidi na mamlaka ili kuweza kufanya kazi ya kuandika na
kuripoti taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Aidha, alisema ni vyema mamlaka ikawa na utaratibu wa kukutana na waandishi
wa habari mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo na pia kubadilishana
mbinu mbalimbali za kutoa taarifa ili pia ziweze kuwavutia wasomaji.
Akifunga mkutano huo Dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru wanahabari hao kwa
michango waliyoitoa na kusema TMA itayafanyia kazi mapendekezo yote
waliyoyatoa. Alitoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuendeleza kazi nzuri
wanayoifanya ya kuwafikishia wananchi taarifa za hali ya hewa kwa wakati.
Aidha alisem a TMA itajadiliana na vyombo vya habari ili kuona uwezekano wa
kuongeza wigo wa utangazaji wa habari za hali ya hewa.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi akifafanua jambo
kwa wanahabari.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...