Baraza la
madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti ya
sh.bilioni 121 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa
Yusuph Mwenda alisema fedha hizo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya
mapato , pesa kutoka ruzuku serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo ya
ndani ya Halmashauri .Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa kujiendesha
kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa ikijiendesha kwa
asilimia 20 tu.
Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo la
kutekeleza mipango ya maendeleo na kuwaondolea umaskini wakazi wa
kinondoni na kuboresha maisha yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni.
Ingependeza km hao Halmashauri ya Kinondoni wangefafanua mfano ktk hizo bil 121 bilioni kadhaa ni kwa ajili ya kitu fulani.
ReplyDeletehii inasaidi hata wakazi wa eneo husika kujua kuwa kuna mpango kazi wa kitu fulani mwaka huu.
mfano. mwaka huu tunaamua kujenga barabara inayo toka sehemu fulani mpaka sehemu fulani.
pia tunatarajia kuiboresha hospitali fulani labda kuwawekea huduma ya X-Ray hivyo wakazi wa eneo hilo hawatakua na haja tena ya kwenda Mwanamala kwa ajiluli ya kupata huduma.