Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kutembelea miradi ya mji wa Mvomero na Mlali, Kata ya Mlali, Tarafa ya Mlali mkoani Morogoro.
Mhe. Makalla ameridhishwa na kiwango cha mradi wa maji wa mji wa Mvomero na mpango kazi wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo.
“Nakubaliana na mpango kazi wenu na ninaamini kuwa mpaka mwezi wa tano, mtakuwa mmekamilisha mradi huu na kukabidhi kazi kwa Serikali na wananchi wa jiji la Mvomero waanze kupata maji”, alisema Mhe. Makalla.
“Napenda kusisitiza mkandarasi aachane na siasa na kurudi mahali pa kazi na kuanza kazi mara moja na kama kuna mambo yoyote, tutakaa chini na kuzungumza wakati kazi ikiendelea. Kinachotakiwa ni mradi kukamilika kwa wakati na maji yapatikane”, aliongeza Naibu Waziri.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji, ameweza kuona hali ya utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali katika mkoa wa Morogoro huku akisisitiza atahakikisha lengo la Serikali kuwapa wananchi wake maji linatimia.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akifungua rasmi mradi wa maji wa Kigugu.
Mhandisi Mkazi akimsomea ripoti ya mradi wa mji wa Movemero, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
Mradi wa maji wa mji wa Mvomero.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa katika kituo cha kusukumia maji cha mradi wa maji Malali.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, akizungumza na wananchi wa Mlali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...