Rais Mstaafu wa Nigeria na Mwenyekiti wa Kamati ya Watu Mashuhuri ya ACP Mhe Olusegun Obasanjo akiongoza kikao cha Kamati ya Watu Mashuhuri wa ACP. Kikao kinafanyika Addis Ababa Ethiopia leo. Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Dr. Leone Reyna, Mhe. Kaliate Tavola, Prof. Sebastio Izata, Prof Ibrahima Fall, Bi. Patricia Francis, Balozi Nureldin Satti, Dr Daoussa Cheriff, Mhe. Kolone Vaai, Mhe Peter Gakunu, Balozi Teshome Toga na Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala. Balozi Kamala amehudhuria kikao hicho kuwakilisha Kamati ya Mabalozi wa ACP.
Kamati ya Watu Mashuhuri wa Afrika, Karibiani na Pacific (EPG-ACP) ambao wanakutana leo Addis Ababa Ethiopia wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Olesugun Obasanjo Rais Mstaafu wa Nigeria. Kamati hiyo inatafakari changamoto, muundo na majukumu mapya ya ACP na mfumo mpya wa ushirikiano wa nchi za ACP, nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya na nchi za ACP na wadau wengine wa maendeleo ifikapo mwaka 2020. Mkataba wa Cotonou ulioweka mfumo wa ushirikiano wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya utakoma ifikapo mwaka 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...