Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu kinachozaniwa ni mlipuko wa bomu uliotokea Jumatatu mchana katika eneo la Mkunazini mjini Zanzibar. Hakuna mtu aliyepata maadhara na hakuna uharibifu wa majengo katika eneo hilo.   

 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe. Abdi Mahmoud Mzee akizungumza naKiongozi wa Kanisa la Mkunazini, Ndg. Nuhu Salanya, na Maofisa wa JWTZ , katika eneo la tukio  alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio waliofika kuagalia na kuchunguza tukio hilo.

Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu. PICHA NA ZANZINEWS 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tuelezwe aina ya bomu?Hakuna CCTV hapo wakajua nani aliweka?

    ReplyDelete
  2. Enyi watu nyeee,kama kweli hilo ni bomu,hicho kijiukuta kilichojengwa kwa mchanga na pengine kwa chokaa kilichopo hapo ambacho kipo si umbali wa futi nne kiwe salama kweli. Lakini si vibaya kuchukuwa tahadhali .

    ReplyDelete
  3. Bomu My foot....wakaulize congo tu hapo how bomu iz look like!!

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na maoni ya wadau watatu wa mwanzo hapo juu. Pengine ni kitu kingine tu kimeripuka lakini kwa kusema bomu, nadhani hicho kiambaza kisinge stahamili kishindo, pengine hata hivyo vibao vya matangazo vingekwenda kuokotewa Vuga. Sema tu kwa vile hiyo eruption imetokea karibu ya hilo Kanisha hapo Mkunazini, basi tena ndo hapoooo!....Pumu imepata mkohozi. Hata hivyo, kama itathibitika kuwa ni bomu, basi tahadhari zaidi za kiusalama zichukuliwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...