MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
serikali inatumia mamilioni kwa siku kwa mambo ya kipuuzi kama katiba , huyu mtoto apelekwe na serikali india angalao akatibiwe , wanasiasa wao kwa chek up tu huenda afrika kusini, marekani , ujerumani na uingereza , mpelekeni huyu mtoto japo india acheni dhuluma , hizo pesa mtazozitoa ni zetu sisi walipa kodi
ReplyDeletejamani malaika wa Mungu.....kwanini nchi isiwe inaangalia watu kama hawa sasa milioni mbili kwa serikali kusaidia mbona ni jambo dogo sana...rais wetu hupo wapi hapo kwa huyo malaika wa Mungu amenisikitisha sana ila ndio hivyo nami sipo vizuri kivile.Nchi za wengine zinavyojali watoto mbona angeishatibiwa mambo mengine yanakuja baadae.
ReplyDeleteMwaisango, hongera sana kwa kutujuza habari hizi za kusikitisha. nafikiri Milioni 2 si kitu sema tu hata wengine tupo maskini lakini tungeweza kutoa tu. Mpigie simu au peleka ombi hilo kwa rais atamsaidia tu, kama aliweza kumsaidia Ray C atashindwa kwa malaika huyo? Tusiitupie sana lawama serikali wakati mwingine wanakuwa hawajapata hizo habari lakini nahisi wakizipata watashudhulika, kumbuka watoto mapacha waliopelekwa india kutenganishwa ni serikali ilifanya hilo kwa njia ya usitawi wa jamii.
ReplyDeleteunajua kila kitu serekali inalaumiwa ingejuaje luna mtoto ana tatizo kama hilo. Huyo mganga alimtibu mara ya mwisho hakuona huyu mtoto anahitaji huduma ya kitalaamu zaidi akampa rufaa jamani? nina imani watoto hawahitaji bima ya matibabu. huyu mtoto atakuwa vizuri kabisa kama mkondo wa huduma ukifuatwa kpale hawpawezi apelekwe India au popote kama wanavyopelekwa wengine acheni ukiritimba mtoto ahudumiwe
Deletekuna uzembe ulitendeka katika kumhudumia huyu mtoto hii hali ingezuilika kama wangechukua hatua ya kuhamishia huduma yake kwa watalaam. badoi hajachelewa ustawi wa jamii changamka huyu mtoto ahudumiwe. pengine mlikuwa hamjui vyombo vya habari vimeshaweka wazi kinachotakiwa hapa huduma na sio kusema raisi yuko wapi wahusika wawajibike au la wawajibishwe.
Deletepoleni sana kwa hili tatizo.
ReplyDeletesikubaliani na mchangiaji wa tatu hapo anasema serikali haiwezi kulaumiwa , kwani huyu mtoto katoka nje ya nchi? aliungua nchi ya kigeni? jee hakutibiwa hospitali ya serikali mpaka akapona hayo makovu? muda wote hao wanaowakilisha serikali hawakumuona? acha kujipendekeza ndugu yangu kwa serikali rushwa , yule aliyepelekwa india kutenganishwa kulikuwa na namna kama kawaida na ulaji mkubwa umepita , fedha zilitumika kumtibu mtoto yule ni ndogo kuliko walizodai kuwa zimetumika kwenye bajeti zao, maofisa wetu serikalini hutumia shida za watu kujinufaisha ,
ReplyDeletewachangiaji msilumbane nina imani wahusika wamesikia na wameona hali ya mtoto ombi letu ni mtoto kuhudumiwa. sidhani kama kuna mtu anajipendekexa hapa anajaribu kuondolea watanzania dhana potovu ya kulaumu badala ya kuchangia hoja in a constructive way. Ndio maana mwana blog anaonya usichafue hali ya hewa ktk uchangiaji. Jamani malaika ahudumiwe sio ajabu ni Makufuli wa kesho
ReplyDelete