Mtangazaji, Dj na Producer wa Kituo cha Radio MAMBO JAMBO (MJ) FM Arusha Hamis Abtway Maarufu kama DJ Haazu amezindua rasmi Tovuti (Website) yake mpya inayolenga Kuukuza Mziki wa Tanzania na Afrika Mashariki Kiujumla.
Website hiyo itakuwa ikitoa Update za Habari za Burudani zaidi, nyimbo Mpya na Video za nyimbo za Nyumbani kuzipeleka kimataifa zaidi huku pia ikiwa haiachi kukupa Habari za Burudani za Kimataifa ili kuonyesha Utofauti wao na wetu ili kujua Tunafanyaje kufikia Level ya Kimataifa Kwa kushirikiana na wadau na Website zingine Pendwa Nchini.
Kupitia website hiyo Haazu ana imani kubwa kuukuza Mziki wetu kwa kiasi kikubwa kutokana na Network aliyo nayo kwa sasa huku pia watu wakizipata Habari zote zitakazokuwa zikitoka kwenye Vipindi vyake Vyote anavyoviendesha MJ FM kama vile DUNDO, EA MIX nk.
UNAWEZA KUTEMBELEA WEBSITE HIYO HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...