mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira
Na Valence Robert-Geita
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.
Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa mahojiano zaidi.
Kuna makabila au mataifa ambayo hayaruhusu mtoto kwenda shule. Huyu binti anaweza kuja kuwa mke wa rais baadaye. Si vuzuri Akawa ni dada mbumbumbu kichwamaji na kuleta aibu kwa taifa. Hongera mzazi kwa juhudi binafsi ila punguza hasira na kutumia nguvu kutimiza wajibu wako.
ReplyDeleteMzee wa busara
huyu baba nafikiri yeye mwenyewe ni mwehu kichaa kasorobo hafai hata kufuga kuku mbali kulea mwana
ReplyDeleteHuyu baba aburuzwe nae, ujinga kabisa. Tunahitaji kuelimisha watu jamani.
ReplyDeletevizurio siku nyingine hatakataa kwenda shule. Shule ndio msingi wa maisha.
ReplyDeleteKama siamini stori hii.Nahisi imetiwa chumvi mno kiasi kuleta msisimko kwa waisikiao.Jamani mtoto akokotwe kwa pikipiki mtaa mzima lakini asichunike popote,nguo isichanike,na bado mtoto ang'are . Iko namna hapa,mimi nahisi ukweli wa chumvi hii sio wakawaida. Yafaa papimwe hapo katika chumvi hii jamani,haifai jazba.
ReplyDeleteKwa upande mwingine wa sarafu ....Baba mtoto anajua machungu ya kukosa elimu! ila mmmh!
ReplyDeleteNingekua karibu ningempa uyo baba zawadi ya gunia la mchele, uyo mtoto hajui kiasi uyo baba anaumia anapokua ziwani anavua samaki, anapata mateso yote hayo kwaajili yakumsaidia uyo binti, kwa maisha ya Tanzania sasaivi elimu ni muhimu sana sana ili mtu afanikiwe, anayeleta mchezo na shule anapaswa kupewa adhabu kali mana matokeo yakutokwenda shule ndo majambazi na wala rushwa wabadae.
ReplyDeleteHekoo kwa uyo baba.
Nyie mnaomsifia huyo baba kumfanyia ukatiri mtoto kiasi icho siwaelewi.
ReplyDeleteNakubaliiana na nyie kwamba mzazi anawajibu wa kuhakikisha mtoto anawkwenda shule na ni kweli elimu ni ya muhimu.
Kukataa Kwa mtoto huyu kwenda shule kunaweza kuwa na sababu ambazo zinabidi zifatiliwe kiundani. Je inawezekana kwamba hayamudu masomo anapigwa mijeredi na walimu kila siku? Tunajua walimu wetu walivyo mtoto akiwa haelewei hawamusaidii Kwa kumfafanulia ila Kwa viboko.
Je inawezekana anasumbuliwa na wanafunzi wenzake (bullied) nayo inaweza kumfanya asiipende shule. Na huyo mzazi kama ameamua kumhadhibu mtoto Kwa njia hii inawezekana binti hana maisha mazuri nyumbani hivyo inaweza kuchangia kutopenda shule.