Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Mh.Dkt.Christine Ishengoma akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ghala la Mazao,katika kijiji cha Kaning`ombe,wilayani Iringa mkoani humo mwishoni mwa wiki,wakati wa uzinduzi wa mwaka wa Kilimo wa Afrika.
Sehemu ya Wadau mbalimbali wa kilimo walioshiriki uzinduzi huo wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika mkoani Iringa.
Mwakilishi wa shirika la Afrika One kutoka Afrika Kusini,Mercy Erhiawarien akitoa ufafanuzi mbele ya wadau wa kilimo (hawapo pichani),kuhusiana na namna kilimo kinavyoweza kuwasaidia Watanzania,hasa kwa vijana na akina mama.
|
Pichani juu na chini ni Mabalozi wa Kilimo nchini,Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay pamoja na mchora katuni maarufu nchini,Masoud Kipanya wakizungumza mbele ya Wadau (hawapo pichani) namna kilimo kinavyoweza kuwakomboa vijana.
Baadhi ya Wadau Viongozi wakifanya Ukaguzi wa shamba la mfano katika kijiji cha Kaning'ombe,waliayani Iringa mkoani humo.
|
Wasanii ambao ni Mabalozi wa Kilimo nchini, Mrisho Mpoto na Profesa J ambao ni mabalozi wa kampeni ya "Kilimo Kinalipa, Jikite" walikuwepo
|
sehemu ya shamba la mfano la mkulima mdogo,Mzee Mbagile.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...