Bw Kiswaga akiwashukuru wana kalenga
kwa maombi na imani yao kwake.
Na Francis Godwin, Iringa
Wakati leo wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM jimbo la Kalenga wanakutaka katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa kumteua mgombea ubunge kupitia CCM katika jimbo la Kalenga wana Kalenga wasema isingekuwa demokrasia kwa kila mmoja kugombea basi wangempitisha moja kwa moja Jackson Kiswaga kuwa mbunge wao
Wamesema jitihada zake za kimaendeleo katika jimbo la Kalenga na mkoa wa Iringa ni kubwa na hakuna mgombea hata mmoja kati ya tisa waliojitokeza ambae anaweza kumfikia Kiswaga katika kujitolea kwa shughuli za kimaendeleo jimbo la Kalenga na mkoa wa Iringa .
Wameongezea kuwa Samson Kalinga kuwa hata wakati wa uhai wake mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa alipata kumpongeza kwa kuonyesha ukeleketwa wa kweli wa maendeleo ya wana Kalenga kwa kuchangia shughuli mbali mbali za kimaendeleo .
Hata hivyo alisema imani ya wana kalenga ni kuona wana CCM hao leo wanamchangua mtu mwenye malengo ya kweli ya kuwakomboa wana Kalenga kama ilivyo kwa Kiswaga na si vinginevyo .
Kiswaga amepata kujitolea kuchangia sekta ya elimu kwa kujenga madarasa katika shule ya sekondari Lipuli, kununua vitanda vya kujifungulia wakina mamaa Hospital ya Ipamba , kuchangia madawati na umeme shule ya msingi Tanangozi ,kuchangia madawati shule ya msingi Lulanda na maeneo mengine mengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...