Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi majina ya Bar 10 yaliyofanikiwa kuingia fainali katika shindano la uchomaji nyama kwa mwaka 2014 lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2014”.
Shindano hili linalofanyika kila mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar Es Salaam. Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo. Kwa mwaka huu baa 10 zilizopigiwa kura kwa wingi(Top 10 Bars) ni New City Pub kura 2519, Kalembo Bar kura 2161, Bonanza Bar kura 455, Blue House kura 353, Rombo Deluxe kura 319, Nebana Bar kura 275, Tarakea Bar kura 247, Savoy Bar kura 139, Mbeya City Pub kura 122 na Iwawa Bar kura 107.Jumla ya Bar 45 zilipigiwa kura kwa Mkoa wa Mbeya.
Baa tano zilizopata kura nyingi zaidi zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakalofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba zikikisindikizwa na burudani ya muziki wa Bendi ya hapahapa Mkoani ya TOT. Baa hizo ni New City Pub yenye kura 2519, Karembo Bar yenye kura 2161, Bonanza Bar yenye kura 455, Blue House Bar yenye kura 353 na Rombo Deluxe yenye kura 319.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Nyanda za juu Kusini, Cloud Chawene, , “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.
Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 2, Mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe ama CCM Ilomba kuanzia saa nne asubuhi ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili
Bwana Cloud Chawene alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma pale wanapoihitaji. Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu. Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”. Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Bila Safari Lager, Nyama Choma haijakamilika!.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...