JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA KWA UMMA
RATIBA YA UZIMAJI WA MITAMBO YA UTANGAZAJI YA ANALOJIA AWAMU YA
PILI
Ndugu
wananchi, napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa Awamu ya Pili ya Uzimaji
wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza rasmi mwezi Machi mwaka huu. Awamu
hii ya Uzimaji inaanza baada ya Serikali kujiridhisha na matokeo ya tathmini ya uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia
awamu ya kwanza kwenye miji saba ya Dar
e salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Moshi na Arusha. Tathmini hiyo imeonyesha
kuwa asilimia 89% ya watanzania kwenye
miji hiyo wamehamia kwenye mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.
Ninaamini
kuwa asilimia kumi na moja ya
watanzania waliobaki kwenye miji hiyo watakuwa wameingia katika mfumo wa dijitali
hadi hivi sasa.
Ndugu
wananchi, Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza mwezi Machi mwaka huu katika miji
tisa na kukamilika mwezi Oktoba 2014. Miji hiyo ni Singida, Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma, Morogoro, Kahama, Iringa na
Songea.
Natoa
wito kwa wadau na wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kutekeleza vema
zoezi hili la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia kwa manufaa ya Taifa
letu na wananchi wote kwa ujumla.
Asanteni sana.
Imetolewa na:
Prof. Makame M. Mbarawa (MB.)
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia
DAR ES SALAAM
21/02/2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...