TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 07.02. 2014.
·
WATU 03 WA FAMILIA MOJA
WAFARIKU DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA UKUTA MKOANI MBEYA.
·
WATU 07 WAKAMATWA NA JESHI LA
POLISI MKOANI MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
WATU 03 WA FAMILIA MOJA
WAFARIKU DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA UKUTA MKOANI MBEYA.
watu watatu wa familia moja waliotambulika kwa majina ya steven mwaijombe (35) baba wa familia, ester kibona (25) mama wa familia na
mtoto wao edgael steven mwaijombe (02)
wote wakazi wa sogea walifariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba
yao wakiwa wamelala. tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 07.02.2014 majira ya saa
04:45hrs usiku wa kuamkia leo huko eneo la sogea kata na tarafa ya tunduma
wilaya ya momba kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani mbeya. miili
ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya tunduma. kamanda wa polisi mkoa
wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa pole kwa ndugu na majirani wa familia hii
kutokana na janga hilo.
WATU 07 WAKAMATWA NA JESHI
LA POLISI MKOANI MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
jeshi la polisi mkoa wa mbeya linawashikilia watu 07 wakiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] ujazo wa lita 11/2.
katika msako uliofanywa mnamo tarehe 06.02.2014
majira ya saa 19:30hrs usiku huko
mwanjelwa na mafiata jiji na mkoa wa mbeya emanuel
mbwete (27) mkazi wa makunguru akiwa na wenzake 05 walikamatwa wakiwa wanakunywa pombe haramu ya moshi. pia
katika msako mwingine hamasha paulo (25)
mkazi wa forest mpya alikamatwa akiwa anakunywa pombe ya moshi. taratibu za
kuwafikisha mahakamani watuhumiwa zinafanyika. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya
kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed
z. msangi anatoa wito kwa jamii hasa vijana kuacha matumizi ya pombe haramu
ya moshi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Nimesikitishwa na hiyo taarifa, haijakaa kiumakini, haijawa edited, taarifa ni ya kiswahili lakini imechanganywa na kiingereza...this is not professional kwa kweli
ReplyDeletena wewe mdau wa namba moja umechanganya kiingereza na kiswahili. unakosoa nimi na unafanya nini? ni kweli taarifa iandikwe kwa kiswahili fasaha nakuunga mkono mdau. ni jukumu la wahusika kuliangalia hilo. kazi njema
ReplyDelete