Mwenyekiti wa Muda wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Pandu Ameir Kificho akiwashukuru wajumbe wa Bunge hilo baada ya kuchaguliwa.
 Muonekano wa Ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba wakati wajumbe wakisubiri kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa muda
 Mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba
  Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akifafanua jambo  kabla ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mchungaji Christopher Mtikila akitoa maoni yake baada ya uchagizi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.
 Kamati ndogo ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba chini ya uongozi wa Mhe. Pandu Ameir Kificho (kushoto). Kamati hii itakayoongozwa na Mhe. Costa Mahalu na Mhe. Magdalena Rwebangula itafanya kazi ya kuichambua rasimu ya Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katib
 Katibu wa Bunge la Muungano Dk Thomas Kashilillah (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Muda Mhe. Pandu Kifico wakati Kamati maalum ya Kanuni ilipokutana. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe ishirini.Picha na Prosper Minja - Bunge Maalum la Katiba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu,jamani naona kama kuna mzungu hapo au macho yangu yana makengeza?,,nao hao waliosema waongezwe hiyo mihela naomba waondolewe maana haiingii akilini mtu ile kuchaguliwa tu cha kwanza alichokiona kuongezewa hihela amakweli nakubaliana na msemo usemao kusoma sn wala sio sababu ya kuwa na mijiakili mingi,,yaani wengi wa watanzania wananjaa kali isiosemekana mijitu mingine ilioaminiwa na wanachi pamoja na RAIS wetu lakini wapi siku tatu tu ashasahau yakwamba uongozi ni dhamana mtakufa bila kujiguna lo mshindwe nyie

    ReplyDelete
  2. Kiswahili ni lugha inayoendelea kuenea kwa kasi Afrika. Baadhi ya nchi za maziwa makuu Afrika Mashariki imekuwa ni ngao yao katika janga la kubaguana kikabila katika nchi zao, japo baadhi ya nchi hizo kwa ajili ya ubaguzi wao ulio ndani ya damu zao wanakikandia kiswahili eti ni lugha ya kimalaya na utapeli.
    Sasa sisi WaTanzania tunaokielewa kiswahili na maana yake halisi halafu tunakielekeza mwelekeo wa tabia isiyo njema kwa kutamani fedha katika kazi ya kutunga sheria za Bunge letu Maalum la k Katiba yetu mpya na tunasahau kutetea hali halisi na sura ya nchi yetu mbele ya watu wengine na watu wetu tutamlaumu nani?
    Wabunge wa Katiba wanataka kupata posho kubwa bila kujali kuwa Tanzania yao ni nchi maskini na wao wanatakiwa kuisaidia Tanzania katika kutunga sheria za kuikomboa katika hali hiyo ngumu, lakini badala yake wanajijali wao kwanza. Hali kama hii ni sawa na tabia fulani ambayo hutokea kwa baadhi ya WaTanzania wenzetu wanaotupa watoto wanaowazaa ili wasiwe na jukumu la kulea na wao waendelee na maisha yao. Hii ni tabia ya kiswahili yenye maneno mengi lakini vitendo hamna. Watu wengine hawapendi maneno mengi na tamaa zisizo na maana kama hizi katika Bunge letu la kutunga sheria wanazozidai nikiwemo mimi. Ni tabia ya ulaji tu, hakuna kingine. Tuwe Wazalendo. Mungu Ibariki Tanzania.
    -Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...