Habari na picha na 
Frank Shija - Maelezo 
 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekanusha taarifa zilizodai kuwa kumegunduliwa Gesi na Mafuta katika maeneo ya Kilosa, Kilombero,Tanga na Maeneo ya Kilimanjaro kwa kudai kuwa taarifa hizo siyo za kweli. 
 Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini na taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu upatikanaji wa nishati hiyo na kuongeza kuwa hili upatikanaji wa mafuta udhibitishwe ni lazima kuchimba kisima au visima vya utafiti katika eneo husika. 
 Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mpaka sasa hakuna hata kisima kimoja kilichochimbwa katika maeneo hayo hivyo, ata hivyo amekiri kuwa kumekuwa na zoezi la utafi wa awali ambapo takwimu zimechuliwa na kubaini kuwa upo huwezekano wa kuwepo kwa nishati hiyo hivyo ni vyema wananchi wakasubiri utafi ukamilike ndipo taarifa rasmi ya uwepo wa nishati hiyo itakapotolewa. "Nduguza Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania tunapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa zilizotolewa sio sahihi.
"Tunaomba wananchi wajue kuwa ili kuwa na uhakika kuwa eneo fulani lina mafuta au gesi ni lazima kuchimba kisima/visma vya utafiti katika eneo husika na kuona gesi au mafuta yakitoka yenyewe kwemye kissima au visima hivyo na si vinginevyo". Alisema Killigane. 
 Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa mpaka sasa jumla ya visima vya utafiti wa mafuta vipatavyo 75 vimechimbwa huku ni asilimia 40 tu ndivyo vyenye gesi na vyo ni katika maeneo ya Mkuranga, Songosongo, Ntorya, Mnazi Bay (Mtwara) na Bahari ya kina kirefu. 
 Kwa upande wake Kaimu Kurugenzi wa Utafutaji, Uzalishaji na Huduma za Ufundi Dkt. Emma S. Msaky amesema kuwa suala la upatikanaji wa mafuta katika maeneo mbalimbali hapa nchini linaausisha utafiti wa kiani hivy ni vyema wananchi wakawa makini ili kuepuka kupewa taarifa zisizo sahihi na pengine zina malengo yaliyojificha ndani yake.
 Dkt. Emma aliongeza kuwa mara baada ya utafiti kukamilika na kugundulika kwa rasilimali hiyo ya mafuta, mwenye mamlaka ya kuujulisha umma juu ya uwepo wa rasilimali za mafuta na gesi asilia ni Waziri wa Nishati na Madini na siyo taasisi wala mtu mwingine yeyote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane akiwaonyesha waandishi wa Habari(hawapo pichani) ramani ya utafutaji wa Gesi na Mafuta leo jijini Dar es Salaam.

Picha zikionyesha eneo la bahari lilogunduliwa Gesi na mafuta na ambapo baadhi ya visima vimechimbwa. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji, Uzalisha na Huduma za Kiufundi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. Emma S. Msaky(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna visima vya utafiti wa mafuta na Gesi vinavyochimbwa leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mtaalamu wa Jeolojia Bw. Simon Zabron.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii controversial ililetwa na baadhi ya viongozi katika baadhi ya mikoa husika, so it is a shame when a tail doesn't know what a head is thinking.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...